Serikali ya
Tanzania imesema ajira za walimu wapya zitaanza rasmi Mei Mosi, mwaka huu 2015
huku ikiweka wazi kuwa walimu hao wasitegemee kupangiwa katika maeneo ya
majiji, manispaa na miji.
Walimu hao
wametakiwa kutotegemea kupangiwa katika maeneo hayo kutokana na idadi ya walimu
waliopo ni kubwa na inakidhi mahitaji, huku maeneo yaliyopewa kipaumbele ni
vijijini na halmashauri ambazo zina mahitaji na upungufu mkubwa wa walimu.
Idadi ya
walimu wapya watakaoanza ajira zao mwezi ujao ni 31,056 ambapo kwa walimu wa
ngazi ya Cheti ni 11,795, Stashahada (Diploma) 6,596 na wenye Shahada (Degree)
12,665.
Hayo
yameelezwa jana April 13,2015 na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu ajira mpya za walimu kwa mwaka 2014/2015.
Alisema kwa
mwaka huu ajira hizo zimechelewa kutokana na TAMISEMI pamoja na Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi kufanya ufuatiliaji wa kina hadi katika ngazi ya shule ili
kubaini kwa uhakika mahitaji halisi ya walimu kwa kila halmahauri na shule.
“Ufuatiliaji
huo umebaini kuwepo kwa halmashauri na shule hasa za mjini zenye walimu wa
ziada na zingine hasa za vijijini zina upungufu mkubwa wa walimu,” alisema
Sagini.
Alisema
taarifa hizo zimesaidia kuwapanga walimu wapya kwa usawa ili kuondoa uwiano
usioridhisha kwenye maeneo mengi ya vijijini. Alisema kwa sasa wanakamilisha taratibu
za kupata kibali kwa ajili ya ajira za walimu na fedha za kuwalipa stahili zao
ili waanze ajira zao rasmi mwezi ujao.
Aidha,
alisema orodha ya walimu na vituo watakavyopangiwa vitawekwa katika tovuti ya
Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ambayo ni www.pmoralg.com na ya Wizara ya Elimu
www.moe. go.tz ifikapo Aprili 24, mwaka huu.
Kwa upande
wake Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Zuberi Samataba alisema, pia ufuatiliaji
huo ulikuwa ni kuhakikisha wanakuwa na taarifa sahihi za walimu wanaoajiri wote
ni wapya ambao hawajawahi kuajiriwa ili kuepuka usumbufu kwa walimu ambao
hawatoi taarifa.
Alisema
baadhi ya walimu ambao wameshaajiriwa wanapoenda kusoma, hupangiwa upya vituo
na hawatoi taarifa hivyo kuleta usumbufu wa kuchelewa kutopata mishahara yao.
“Kuna baadhi
ya walimu wameshaajiriwa kwa hiyo jina linapoingizwa katika taratibu za malipo,
linagoma kuingia ndipo ukifuatilia unajua alikuwa ameajiriwa, inabidi umwambie
arudi kwa mwajiri wake.
Kwa hiyo kwa
hawa walimu wapya nawashauri waende kuripoti katika vituo walivyopangiwa na
wakubali kufanya kazi katika maeneo hayo, sio waripoti halafu waondoke,”
alisema.
|
Tuesday, April 14, 2015
Home
HABARI
AJIRA YA WALIMU:-Rasmi Mei 2015 na Wasitegemee kupangiwa katika maeneo ya majiji, manispaa na miji.
AJIRA YA WALIMU:-Rasmi Mei 2015 na Wasitegemee kupangiwa katika maeneo ya majiji, manispaa na miji.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment