Mwalimu Veronika Mtes wa shule ya msingi
Kibirizi ,Manispaa ya Kigoma/Ujiji aliyepata mshtuko baada ya tukio la radi akiwa katika hospitali ya
Mawenzi mkoa wa Kigoma kwa matibabu. |
Mwalimu Merina Sekilo aliyenusurika kupigwa na radi wakati akifundisha darasa la kwanza,ambapo wanafunzi 6 walifariki. |
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Kigoma,Maweni
akiongeza na Waandishi wa habari juu ya tukio la radi lililotokea hivi
punde na kuuwa watu 8.
Na Editha
Karlo Karlo wa blog ya jamii,Kigoma.
WATU wanane
wakiwemo wanafunzi sita na mwalimu wa shule ya msingi kibirizi mmoja pamoja na
mtu wa kawaida mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapa wamekufa baada ya kupigwa na radi huku
wanafunzi wengi 15 wakijeruhiwa na radi hiyo mchana huu.
Mganga
mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Kigoma (MAWENI) Dkt Fadhili Kabaya alisema kuwa
watu hao walifikwa na mauti hayo kufiatia mvua kubwa zilizonyesha zikiambana na
radi zilianza majira ya saa sita mchana.
Dkt Fadhili
aliwataja waliokufa katika tukio hilo kuwa ni pamoja na mwalimu wa shule ya
msingi kibiriziElinaza Mbwambo(25)mtu mwingine wa kaida ni Forcus
Ntahaba(45)mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapa.
Aliwataja
wanafunzi waliofariki ambao wote ni wa darasa la kwanza kuwa ni Yusuph
Ntahoma(8)Hassan Ally(9)Fatuma Sley(7)Zamda Seif(8)Shukranmi Yohana(7) na
Warupe Kapupa(10).
Alisema
walipokea majeruhi kumi na tano lakini kati yao kumi wametibiwa na kuruhusiwa
kurudi nyumba baada ya hali zao kuwa nzuri na watano wamelazwa wanaendelea na
matibabu katika hospital ya Mkoa wa Kigoma.
Akisimulia
tukio hilo mwalimu aliyekuwa anafundisha darasani Mwalimu Merina Sililo alisema
kuwa akiwa darasani akiendelea kufundisha ghafla aliona wingu zito jeusi limetanda
hadi akashindwa kuendelea kuandika ubaoni.
''Manyunyu
yalianza kidogo kidogo ikaja mvua kubwa na radi pamoja na miungurumo mikali
sana iliyopelekea wanafunzi kuanguka ovyo darasa na kuzima na mara niliona moto
umetanda katika chumba kuzima cha darasa na mimi nilianguka chini na kupoteza
fahamu''alisema mwalimu huyo.
Alisema
apozinduka alijikuta katika hospital ya Mkoa wa maweni akipatiwa matibabu baada
ya kuletwa kwa msaada wa waalimu wenzie.
''Kwakweli
ni mungu tu mwenyewe ndo ameninusuru kwani nilirushwa mmara tatu na radi na
watoto wote wote darasani walikuwa wananiangukia mimi wengine walikuwa
wanakimbia ovyo nje''alisema Mwalimu huyo.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment