Katibu mkuu
wa Wizara ya Tamisemi Jumanne Sagini akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani).
Serikali
imewataka Makatibu Tawala wa Mikoa ambayo shule zake zimefungwa kwa madai ya ukosefu
wa chakula, kuwachukulia hatua Wakuu wa shule hizo, kwa kile kilichoelezwa kuwa
wamekiuka utaratibu kutangaza hivyo ilhali Serikali ilishatuma fedha kwa ajili
ya chakula cha wanafunzi katika shule mbalimbali nchini.
Shule
zilizofungwa kwa tatizo hilo na mikoa yake kwenye mabano ni Rugambwa, Kahororo,
Nyakato na Ihungo (Kagera), Lyamungo (Kilimanjaro), Mpwapwa na Abeid Karume
(Dodoma), Kazima, Milambo, Wavulana Tabora na Wasichana Tabora (Tabora).
Uamuzi huo
umetangazwa Jana April 13,2014 na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini aliyesema serikali imeshatoa asilimia 66.7
ambazo ni Sh bilioni 28.1 zilizotengwa kwa mwaka 2014/2015.
Alisema
serikali imetoa fedha hizo katika kipindi cha mwezi Julai mwaka jana 2014 hadi Machi
mwaka huu 2015 kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa shule za sekondari,
zinazomilikiwa na serikali. Sagini alisema serikali ilitenga Sh bilioni 42.1
kwa mwaka 2014/2015, ambapo kati ya fedha hizo kiasi kilichobaki ni Sh bilioni
13.9, sawa na asilimia 33.23 ya fedha zilizotengwa.
“Kwa ufupi,
serikali haijafunga shule na wakuu wa shule waliotangaza kufunga shule hizo
chache wamefanya makosa kwa kuwa hawakuwasiliana na mamlaka husika ili kupata
kibali kama kungekuwa na sababu ya kufanya hivyo, naamini mamlaka husika
zitawachukulia hatua,” alisema Sagini.
Alisema
wamiliki wa shule ni Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambazo watendaji wake ni
wakurugenzi na wakuu wa shule ni viongozi wasimamizi wa shule hizo, hivyo
hawana mamlaka ya kutangaza kufunga shule kwa sababu yoyote bila kibali cha
mwenye shule.
Kwa mujibu
wa Sagini, kuna utaratibu wa kufunga shule ambapo katika kipindi hiki, shule
nyingi zilikuwa zimefungwa kwa mapumziko mafupi kati ya Machi 28 hadi Aprili
12, ambapo katika shule hizo zilizofungwa wanafunzi walilazimika kurudi makwao
kutokana na kutangaziwa na wakuu wao wa shule.
|
Tuesday, April 14, 2015
KUFUNGWA SHULE KISA CHAKULA:-Wakuu wake Kukiona cha Moto.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment