FA CUP :-Arsenal sasa hao Fainali kuwasubiri Kesho Jumapili April 19, 2015 kati ya Aston Villa au Liverpool. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 18, 2015

FA CUP :-Arsenal sasa hao Fainali kuwasubiri Kesho Jumapili April 19, 2015 kati ya Aston Villa au Liverpool.


Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Arsenal Leo hii April 18, 2015 wakicheza Uwanja wa Wembley Jijini London, wameichapa Timu ya Daraja la chini la Championship, Reading  Bao 2 - 1 katika Nusu Fainali ya kombe hilo.

 Pasi safi ya Mesut Ozil ndiyo iliyompa nafasi Alexis Sanchez kuipa Bao la kwanza Arsenal Dakika ya 30 Bao ambalo lilidumu hadi Mapumziko.


 Reading walisawazisha katika Dakika ya 54 kwa Bao la McCleary  alieunganisha krosi ya Pogrebnyak kutoka kushoto kwa goli. 

Hadi Dakika 90 kumalizika Gemu ilikuwa 1-1 na kuongezwa Dakika za Nyongeza 30.

Alexis Sanchez aliipa Arsenal Bao la Pili na la ushindi katika Dakika ya 106 baada ya Shuti lake kumpenya Kipa Federici.

Nusu Fainali nyingine itachezwa Kesho Jumapili April 19, 2015, pia Uwanjani Wembley, kati ya Aston Villa na Liverpool.KUCHEKI PICHA ZAIDI ZA MCHEZO HUU..BOFYA HAPA

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad