AMANI,SALAMA NA USHIRIKIANO:-Taswira Picha wakati wa sherehe za miaka 51 ya Muungano zafana jijini Dar es salaam leo April 26,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 26, 2015

AMANI,SALAMA NA USHIRIKIANO:-Taswira Picha wakati wa sherehe za miaka 51 ya Muungano zafana jijini Dar es salaam leo April 26,2015.

Rais Dk. Jakaya Kikwete na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa katika maadhimisho ya muungano.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete leo April 26,2015 amewaongoza Watanzania katika maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali.

 Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa na Viongozi wengine wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, leo  April 26,2015 kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, leo April 26,2015. Picha na OMR.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad