MATOKEO YA MECHI ZA APRIL 25,2015:-Tazama Hapa ni Manchester City,Liverpool na FC Barcelona pamoja na Ratiba ya gemu za leo Jumapili April 26. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 26, 2015

MATOKEO YA MECHI ZA APRIL 25,2015:-Tazama Hapa ni Manchester City,Liverpool na FC Barcelona pamoja na Ratiba ya gemu za leo Jumapili April 26.


Wachezaji na Kipa wao wa Timu ya Aston Villa wakiwa hawaamini  kilichotokea baada ya Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero kufunga bao lake la 20 katika Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu 2014/2015 katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Aston Villa Uwanja wa Etihad. 

 Mabao mengine ya City yalifungwa na Aleksandar Kolarov na Fernandinho, wakati wa Villa yalifungwa na Tom Cleverley na Carlos Sanchez. 

Matokeo hayo yanaipandisha timu ya Man City juu ya Manchester United na Arsenal nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu.

Beki wa West Brom, Craig Dawson akimdhibiti mshambuliaji wa Liverpool, Raheem Sterling kwa kumvuta jezi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza jioni ya jana April 25, 2015 kwenye Uwanja wa The Hawthorns. 

Timu hizo zilitoka 0 – 0 na kuwafanya  Liverpool waanza kupoteza matumaini ya kumaliza ndani ya 4 Bora za Ligi Kuu ili wacheze Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao huku Steven Gerrard, ambaye ni nahodha wa  Liverpool, aliiongoza Timu yake ikiwa ni Mechi yake ya 500 ya Ligi na pia Mario Balotelli kuanza Mechi yake ya kwanza tangu Februari lakini hawakupata ushindi.

Matokeo haya yamewabakisha Liverpool Nafasi ya 5 wakiwa nyuma ya Timu ya 4 Man City ambao wako Pointi 6 mbele.

Msimamo-Timu za Juu EPL 2014/2015.

RATIBA EPL

Jumapili Aprili 26,2015.

1530 Everton v Man United

1800 Arsenal v Chelsea

Jumanne Aprili 28,2015.

2145 Hull v Liverpool

Jumatano Aprili 29,2015.

2145 Leicester v Chelsea


Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar akijaribu kumtoka mchezaji wa Espanyol, Alvaro Gonzalez (kushoto) katika mchezo wa La Liga jioni ya jana April 25, 2015 kwenye  Uwanja wa Cornella-El Prat, au Power8. 

Barcelona ilishinda 2-0 mabao yake yakifungwa na Neymar dakika ya 17 na Messi dakika ya 25 na ushindi huo kuwafanya sasa Barcelona kufikisha pointi 81 baada ya kucheza mechi 33, ikiizidi kwa pointi tano Real Madrid.

LA LIGA 2014/2015.


Msimamo-Timu za Juu.

1. Barcelona Mechi 33 Pointi 81

2. Real Madrid  Mechi 32 Pointi 76

3. Atletico Madrid Mechi 33 Pointi  72

Real Madrid wao wanacheza leo April 26, 2015 Jumapili Ugenini na Celta Vigo Timu ambayo waliichapa 3-0 katika Mechi ya kwanza.

Mabingwa Watetezi Atletico Madrid, ambao  walipigwa 1-0 na Real Madrid na kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Jumamosi April 25, 2015 walikuwa Nyumbani kucheza na Elche wakiwa tayari wameshapoteza matumaini ya kutetea Taji lao na kushinda bao 3-0.

LA LIGA 2014/2015 RATIBA/MATOKEO.


Jumapili Aprili 26,2015.

1300 Malaga CF v Deportivo La Coruna

1800 UD Almeria v SD Eibar

2000 Sevilla FC v Rayo Vallecano

2200 Celta de Vigo v Real Madrid CF


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad