UTEUZI WA RAIS:-Wabunge wawili waapishwa Bungeni Dodoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 27, 2015

UTEUZI WA RAIS:-Wabunge wawili waapishwa Bungeni Dodoma.

Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Dkt. Grace Puja akila kiapo ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma leo Machi 27, 2015.

Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Innocent Sebba akila kiapo ndani ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma leo Machi 27, 2015.

Wabunge wawili walioteuliwa na Rais Dr.Jakaya Kikwete siku chache zilizopita Dr.Grace Puja na Inocent Sebba leo wameapishwa huku uteuzi wao ukizua mjadala hali iliyomfanya Spika Anna Makinda kumtaka Mwanasheria mkuu wa Serikali kutolea ufafanuzi.

Dakika chache baada ya viapo hivyo mbunge wa jimbo la Muhambwe Felix Mkosamali aliomba muongozo wa spika kuhusiana na madaraka ya Rais kuweza kufanya uteuzi huo ili hali kuna baadhi ya majimbo yapo wazi na uchaguzi haurusiwi kufanyika.

Akijibu muongozo huo mwanasheria mkuu wa Serikali George Masaju amesema kwa mujibu wa katiba Rais anaruhusiwa kuteua wabunge muda wote anaoamua yeye.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Afya Kebwe Steven Kebwe amesisitiza kuwa matibabu yote ya ugonjwa wa kisukari ni bure katika hospitali za umma.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad