UEFA LIGI 2014/2015:-Manchester City yaungana na Chelsea na Arsenal kuaga katika 16 Bora . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 19, 2015

UEFA LIGI 2014/2015:-Manchester City yaungana na Chelsea na Arsenal kuaga katika 16 Bora .


Wachezaji wa FC Barcelona wakimpongeza Ivan Rakitic baada ya kufunga bao pekee dhidi ya Manchester City  katika ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya jana March 18, 2015,usiku.

Rakitic alifunga bao hilo dakika ya 31, akimalizia krosi ya Lionel Messi na sasa Barcelona inafuzu Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1, baada ya awali kushinda 2-1 .





Katika mchezo huo, mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero alikosa penalti dakika ya 78 ambayo iliokolewa na kipa Marc-Andre ter Stegen. Penalti hiyo ilitolewa baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Gerard Pique.

Manchester City imeungana na timu nyingine mbili za Uingereza, Chelsea na Arsenal kuaga katika 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa na sasa zote zitahamia kwenye Europa League.


Jamie Redknapp, Thierry Henry and Jamie Carragher pitch side at the Nou Camp while working for Sky Sports.

Nao Juventus ya Italia imefuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia ushindi wa mabao 3-2 ugenini dhidi ya Borussia Dormund usiku wa jana March 18, 2015  Uwanja wa Westfalenstadion, Dortmund, Ujerumani.

Juventus  sasa inakwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1, baada ya awali kupata ushindi mwembamba nyumbani wa 2-1. 

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Carlos Tevez aliifungia Juve bao la kwanza dakika ya tatu, kabla ya Alvaro Morata kufunga la pili dakika ya 70 kwa pasi ya Muargentina huyo. 

Tevez aliyewahi pia kuchezea Manchester City, aliifungia Juve bao la tatu zikiwa zimesalia dakika 10 na hicho kinakuwa kipigo cha nne kwa Dortmund katika mechi nne walizokutana na Juventus kwenye michuano ya Ulaya.



Arsenal Juzi March 17, 2015, Usiku iliichapa AS Monaco 2-0 kwao Stade Louis II Jijini  Monaco ambako hawajafungwa tangu 2005 lakini wametupwa nje ya UEFA Champions League msimu huu 2014/2015 kwa Bao za Ugenini na hii ni mara ya 5 mfululizo kwa Arsenal kushindwa kutinga Robo Fainali.

Arsenal walifungwa kwao Emirates Bao 3-1 na matokeo hayo kufanya Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili kuwa 3-3 na AS Monaco kutinga Robo Fainali kwa Ubora wa Bao za Ugenini.

Hii ni mara ya kwanza kwa AS Monaco kufika Robo Fainali tangu 2004.

Bao za Arsenal hiyo Jana zilifungwa na Olivier Giroid Dakika ya 36 na Aaron Ramsey, alietoka Benchi, na kufunga Dakika ya 79.

Katika Mechi nyingine iliyochezwa hiyo juzi March 17, 2015 huko Vicente Calderon Jijini Madrid, Wenyeji Atletico Madrid wametinga Robo Fainali kwa Mikwaju ya Penati 3-2 baada ya kufungana Mabao na Bayer Leverkusen 1-1 kwa Mechi mbili.

Leverkusen walishinda kwao Ujerumani,bao 1-0 na Atletico kushinda 1-0 kwa Bao la Dakika ya 27 la Mario Suarez na kudumu hadi Dakika 90 kwisha na hivyo Mechi kwenda Dakika za Nyongeza 30 bila kubadilika.

Atletico, ambao Msimu uliopita wa 2013/2014 walifungwa Fainali ya Mashindano haya na Real Madrid, sasa wanaingia Droo ya kupanga Mechi za Robo Fainali ya UEFA Champions League ,itakayofanyika Ijumaa March 20, 2015 ,saa 7 Mchapamoja na A S Monaco, Real Madrid, FC Porto, Bayern Munich , Paris Saint-Germain,FC Barcelona na Juventus.


UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad