LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Matokeo ya Mechi za Jana March 18, 2015 kwa Simba kugongwa Virungu na Mgambo, Yanga ikirejea kileleni. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 19, 2015

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Matokeo ya Mechi za Jana March 18, 2015 kwa Simba kugongwa Virungu na Mgambo, Yanga ikirejea kileleni.


YANGA SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu 2014/2015 kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo ,March 18, 2015.


Katika mchezo huo, Yanga SC ilikwenda kupumzika ikiwa tayari inaongoza kwa mabao hayo 2-1,kwa bao za Bao za Simon Msuva na Mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita 2013/2014, Mrundi Amisi Tambwe aliifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 15, akimalizia pasi ya Mrisho Ngassa ambaye naye alipasiwa na Kpah Sherman.


Kufatia Ushindi huo wa Pointi tatu, Yanga SC inakuwa imejiweka katika kilele cha ligi kwa alama 35 huku ikiwashusha Azam katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 34.


Nao SIMBA SC  walipunguzwa kasi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kufungwa mabao 2-0 na Mgambo Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga .

Matokeo hayo yanazidi kuondoa matumaini ya Simba SC inayofundishwa na Mserbia, Goran Kopunovic siyo tu kutwaa ubingwa, bali hata kushika nafasi ya pili. 

Mgambo ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa mchezaji wa zamani wa Coastal Union ya Tanga pia, Ally Nassor ‘Ufudu’ aliyemalizia krosi ya Fully Maganga,huku bao la Pili Kipindi cha pili ndipo jahazi la Simba lilipozama kabisa, Bao hilo lilifungwa na Malimi Busungu kwa penalti dakika ya 66, baada ya kipa Ivo Mapunda kumchezea rafu Fully Mganga aliyekuwa anakwenda kufunga.

Ivo alitolewa kwa kadi nyekundu na refa Amon Paul kutoka Mara, na Smba SC ikamuingiza kipa Peter Manyika kwenda kuchukua nafasi ya Said Ndemla.

Katika mchezo mwingine Huko Sokoine, MBEYA City  wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United ya Shinyanga ,mchezo huo ukipigwa  Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mabao ya Mbeya City inayodhaminiwa na kampuni ya Bin Slum Tyres Limited kupitia betri za RB, yamefungwa na Yussuf Abdallah dakika ya 65 kwa penalti na Paul Nonga dakika ya 75.

Ushindi huo unaifanya Mbeya City ifikishe pointi 24 baada ya kucheza mechi 20, wakati Stand inabaki na pointi zake 22 baada ya kucheza mechi 20 pia.

LIGI KUU VODACOM / RATIBA

Jumamosi Machi 21,2015.

Mgambo JKT v Yanga SC

Kagera Sugar v Mtibwa Sugar

Ndanda FC v JKT Ruvu

Ruvu Shooting  v  Simba SC


UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad