Picha ya"Screen
shot" ikionyesha moja ya habari zilizorushwa kwenye moja ya blog uchwara
kuhusiana na taarifa za uzushi wa kifo cha mchungaji Gwajima.
…Ni zile
zinazoandika habari za uongo, matusi.
Na Andrew
Chale wa Modewji blog
Miongoni mwa
mambo ambayo Tanzania tunapitia kwa sasa ni pamoja na teknolojia mbalimbali
ikiwemo mawasiliano ya simu, intaneti vyombo vya habari na mengine mengi,
Lakini mawasiliano hayo kwa sasa ikiwemo Intaneti wapo wanayoyatumia vibaya.
Kupitia
BLOG, mtandao ambao mtu anaweza kutengeneza chombo chake cha kutolea taarifa
ama kufanyaia jambo lolote lile liwafikie wengi kwa mema, lakini kwa sasa hilo
halipo kwani licha ya kuwa kila mtu anaweza kuanzisha blog imetoa mwanya kwa
wengine kuzitumia blog hizo kinyume na matarajio.
Miongoni mwa
mambo hayo ni pamoja na BLOG nyingi ambazo asilimia kubwa mtu yoyote anaweza
kuanzisha tena bure kama ilivyo akaunti yako ya Email, watu wanaoziendesha BLOG
hizo wamekuwa wakiongoza kwa kuweka habari za uongo, upotoshaji, habari
zinazoenda kinyume na maadili, pamoja na habari ambazosi za kweli.
Tunaamini
wapo watu wanaofanya shughuli hizi za BLOG, ambao ni Ma-blogger wazuri tu licha
ya kuwa si wanahabari, lakini kwenye blog zao wana weka ‘POST’ habari nzuri na
zinazoendana na maadili pia wamekuwa wakitoa habari za kuelimisha jamii,
kuifunza jamii na wanapata wasomaji wanaotembelea wengi sana kiasi cha hata
kupewa matangazo na baadhi ya Makampuni binafsi ya kibiashara, Serikali na watu
wengine, lakini shida ni kwenye hizi ‘Blog uchwara’ ambazo kila kukicha wao
kazi yao kukopi na ku-paste habari za kwenye magazeti na kuzipa ‘kiki’ kwenye
blog zao wengine habari hizo hizo za kwenye magazeti wao kazi yao kubadilisha
kichwa cha ‘habari tu ilimradi apate wasomaji wengi?
Jamani kweli hii ni haki?,
tena kichwa hicho cha habari hakiendani na maadili ya Mtanzania ama kinakiuka
maadili hii si sawa, TCRA, muamke na kuchukua hatua kali.
|
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma.
Tunaamini
Mamlaka yaa Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority
(TCRA), (https://www.tcra.go.tz/) mpo na
mnafuatilia lakini sijui kama mnaliona hili ni tatizo ama si tatizo.
Tukumbuke
huko nyuma kulikuwa na mitandao kama hii tena ya watanzania ambao waliifungua
ambapo walianza kuweka picha za kawaida na baadae ikawa inabadilika kuwa
wanaweka picha za utupu… wakaachiwa hivi hivi baadae wakawa wanaweka picha za
viongozi wakiwemo viongozi wakuu wa Nchi mwisho wa siku Mamlaka husika wakaja
kukumbuka shuka wakati mambo yamekua si mambo.
Hivyo ni
wakati sasa kwa TCRA, kuchukua hatua blog zote zinazoendana kinyume na maadili
ikiwemo kupotosha, kuweka pichaa za ngono na kugombanisha watu basi zichukuliwe
hatua.
Mtandao huu
unaamini kuwa na unaungana na wadau wote wanaendelea kutoa maoni yao juu ya
kuzitaka blog hizi zichukuliwe hatua. Kwani mpaka tunaandika habari hii ni
pamoja na baada ya Mdau Yusuph Mhoja kuchukizwa na moja ya habari kwenye
miongoni mwa blog hapa nchini.
(Tazama picha), ambapo Mdau huyo aliuliza: “Hivi
huyu mwandishi anajua kiswahili kweli? Yuko mochwari kwani amefariki huyo?”
wakati anajiuliza hayo, hii ni kuwa inawatokea watu wengi sana wanaapokutana na
habari kwenye hizo blog uchwara.
Wadau
waliochangia mada ya Mhoja: Pendi Mahundi yeye alieleza hivi: “hahaha.... hili
ndiyo tatizo kubwa la kila mtu mwenye kisimu cha TECNO bongo kujifanya blogger
and a self-appointed journalist... UJINGA mtupu, huwa naziona habari kwenye
viblogu mpaka kichefu chefu... full of attention-seeking sensationalism...
utakuta heading: HATARI, Vilio na majonzi, Breaking news, Unbelievable..kisa tu
kutaka watu wazisome blog zao.” Alieleza Mahundi.
Hata hivyo
wachangiaji wengine waliomba serikali kupitisha mswada wa habari na sheria ya
ICT ili kukomesha wandishi wa viblog uchwara.
|
Modewji blog tunaamini pia Mtandao wa wanabloga
Tanzania (Tanzania Blogger Network-TBN) wapo kwani kuna misemo mingi ya zamani
inayosemwa, ikiwemo ule wa SAMAKI MMOJA AKIOZA…? Jibu watatupatiaa TBN ama kama
si lao basi bomu likilipuka tusimtafute mchawi huko mbeleni.
Hata hivyo,
mtandao huu wa Mo dewji blog tunaungana
na TCRA na kusema kuwa: “ #Ukipata ujumbe wa chuki, matusi au uongo, FUTA
DELETE KABISA!.
Tuandikie
maoni yako kupitia kwenye mtandao huu hapo chini ama kupitia simu 0719076376 au
0714940992.
|
No comments:
Post a Comment