LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Baada ya Yanga kushinda 2-0, Coastal na Azam FC,Simba na Ruvu Shooting vitani kesho March 22,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 21, 2015

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Baada ya Yanga kushinda 2-0, Coastal na Azam FC,Simba na Ruvu Shooting vitani kesho March 22,2015.

MABINGWA mara ya 24 wa ligi kuu soka Tanzania bara na Vinara wa Ligi msimu huu 2014/2015 Dar Young Africans wamevunja mwiko wa Mgambo JKT kutofungwa na vigogo Simba SC, Yanga SC kwa misimu mitatu katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga baada ya kuifumua mabao 2-0 katika mechi ya ligi kuu iliyomalizika jioni ya leo March 21,2015.

Mabao ya Yanga SC yamefungwa kipindi cha pili na winga mwenye kasi Saimon Msuva  na mtaalamu wa magoli ya kichwa na mfungaji bora msimu uliopita, Amissi Tambwe.

Bao la leo ni la  9 kwa Msuva na la 5 kwa Tambwe.

Msimu uliopita 2013/2014, Yanga SC walipoteza dira ya kutwaa ubingwa kufuatia kuchapwa 2-1 na Mgambo katika uwanja huu wa Mkwakwani, lakini leo wamelipa kisasi.

Mgambo waliwafunga Simba SC 2-0 jumatano ya wiki hii, lakini leo ,Jumamosi March 21,2015 mambo yamewageukia kwa kula kichapo kama hicho.
Azam fc wakifanya mazoezi jana jioni uwanja wa Mkwakwani. Picha kwa hisani ya Salehjembe.

Kwa Ushindi huo waliyopata Yanga SC wameendelea kujikita kileleni kwa kufikisha pointi 37, pointi nne mbele ya Azam FC  wenye pointi 33 watakaocheza na Coastal Union kesho jumapili March 22,2015 kwenye uwanja huo huo wa Mkwakwani.

Ligi Kuu Vodacom itaendelea pia Siku Jumapili kwa Simba SC walionafasi ya tatu na pointi 29 kuwepo Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shooting wakati Tanzania Prison wako kwao Sokoine Jijini Mbeya kucheza na Polisi Moro.


Hii ilikuwa mechi 18 ya Yanga SC na Azam FC watacheza mechi ya 18 kesho. Kama watashinda wataendelea kuwa nyuma kwa pointi moja na kama watatoa sare watakuwa pointi tatu nyuma ya Yanga SC.


UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad