LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Matokeo ya mechi za leo March 21,2015 Arsenal, Tottenham na Manchester City wakishinda. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 21, 2015

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Matokeo ya mechi za leo March 21,2015 Arsenal, Tottenham na Manchester City wakishinda.

Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Uingereza 2013/2014,Manchester City wakiwa kwao leo March 21,2015,majira ya jioni kupitia  msaada mkubwa wa Refa Neil Swabrick katika Dakika ya Pili alipomtoa Mcheza wa West Brom McAuley kwa Kadi Nyekundu na City kushinda Mechi yao kwa bao 3-0.

Kwenye tukio hilo alieonekana kucheza Rafu ni Dawson lakini Refa alimtoa McAuley.

Ushindi huu umewafanya Manchester City wawe nyuma ya Vinara Chelsea kwa Pointi 3 tu lakini  Chelsea wana Mechi 2 mkononi.

Bao za Man City zilifungwa na Wilfried Bony, likiwa Bao lake la kwanza kwenye Ligi tangu ajiunge Januari, Fernando na David Silva.

Matokeo ya mechi nyingine za leo March 21,2015 ni Newcastle  kufungwa bao 1-2  na Arsenal kwa bao za Olivier Giroud, Tottenham akashinda 4-3  dhidi ya Leicester huku Harry Kane akipiga  hat-trick.

Nao Aston Villa wakafungwa bao 0 -1 na Swansea, Southampton kushinda 2- 0 dhidi ya Burnley wakati  Stoke City  akachapwa bao 1 - 2  na Crystal Palace.

HAPO KESHO JUMAPILI MARCH 22,2015 LIGI KUU.

1630 Liverpool v Man United

1900 Hull City v Chelsea

1900 QPR v Everton


UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad