HABARI ZA HIVI PUNDE:-Buhari aongoza katika matokeo ya awali Nchini Nigeria. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 31, 2015

HABARI ZA HIVI PUNDE:-Buhari aongoza katika matokeo ya awali Nchini Nigeria.

Jenerali Muhammadu Buhari (Kushoto Pichani) anaongoza kwa zaidi ya kura milioni mbili zaidi ya mpinzani wake wa karibu ambaye ni Rais Goodluck Jonathan.

Generali Buhari wa chama cha All Progressives Congress (APC) anaonekana kusajili matokeo mema mapema hata kabla ya kuhesabiwa kwa kura za mjini Lagos. 
Matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Nigeria yanatarajiwa kutangazwa saa chache zinazokuja wakati majimbo yaliyosalia yakisubiriwa kutangaza matokeo yao.

Huku zaidi ya nusu ya matokeo yakiwa yametangazwa mgombea wa upinzani Muhammadu Buhari yuko mbele ya rais wa sasa Goodluck Jonathan.

Hata hivyo matokeo bado hayawezi kutabiriwa kwa kuwa majimbo yenye watu wengi kama Lagos na Rivers hayajatangaza matokeo yake.

Mwandishi wa BBC mjini Abuja amesema mchuano bado ni mkali. 
Tume ya uchaguzi imesema itaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumanne hii ya March 31,2015,asubuhi na kwamba matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa baadaye siku hiyo.

Mwandishi wa BBC anasema yeyote atakayeshinda, litakuwa jambo la kushangaza iwapo mgombea atakayeshindwa hatatamka kuwepo kwa mbinu chafu.

 Source:-BBC Swahili.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad