HABARI / PICHA:-Taswira wakati Benk ya NMB ikizindua Matawi Mapya Tabora na Shinyanga. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 26, 2015

HABARI / PICHA:-Taswira wakati Benk ya NMB ikizindua Matawi Mapya Tabora na Shinyanga.


Tawi la NMB Kishapu.

Benki ya NMB Nchini Tanzania hivi karibuni imezindua matawi mapya mawili yaliyopo kwenye mikoa ya Tabora na Shinyanga. Hii ni habari njema kwa wakazi wa maeneo hayo na kwa wateja wa benki ya NMB kwa ujumla ambapo awali walitembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma za kibenki.

Kuongeza matawi hayo yanamaanisha NMB imewafikia wateja wake katika kila wilaya nchini.

Uzinduzi wa matawi hayo NMB Kaliua na NMB Kishapu yamezidi kuongeza idadi ya matawi ya NMB yaliyotapakaa nchi nzima kuwa zaidi ya 170.

Tawi la NMB Kaliua liko karibu na kutuo cha reli cha Kaliua wakati tawi la Kishapu lipo umbali wa kilometa 49 kutoka barabara ya Shinyanga – Mwanhuzi kutoka Urambo.

Tembelea matawi haya ufurahie huduma na bidhaa mbalimbali zitolewazo na benki yako ya NMB.

Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi - Bw. Abraham Augustino (kushoto) akishangilia pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga - Mhe. Ally Rufunga baada ya kufungua pazia kuashuria ufugunguzi rasmi wa tawi la NMB Kishapu. Picha kwa Hisani ya Michuzi.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad