AJALI YA NDEGE YA GERMANWINGS:- Rubani Lubitz akipata Majinamizi…..’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 29, 2015

AJALI YA NDEGE YA GERMANWINGS:- Rubani Lubitz akipata Majinamizi…..’’

Mwendesha mashtaka mmoja wa Ufaransa anasema rubani msaidizi wa ndege ya kampuni ya Germanwings ambayo ilipata ajali katika milima ya French Alps wiki hii alifanya “jaribio la makusudi la kuiangusha ndege”.


Mwendesha mashtaka wa Marseilles, Brice Robin alisema Alhamis kwamba rubani mwenza, Andreas Lubitz mwenye umri wa miaka 28 alimfungia rubani nje ya chumba cha marubani na kubaki mwenyewe akidhibiti ndege aina ya Airbus A320.

Mwendesha mashtaka alisema Lubitz kisha “aliongeza mwendo na kuishusha ndege kwa  makusudi” ikiruka kwa kasi ya  kilomita 700 kwa saa na kusababisha ajali katika eneo moja dogo kwenye milima yenye theluji huko kusini-mashariki mwa Ufaransa na kuuwa watu wote 150 waliokuwemo ndani.

Ajali hiyo inaweza kutokea tu kwa kufanyika tendo la makusudi”, Robin alisema katika mkutano na waandishi wa habari.  “Kwa namna yeyote ile, ni tukio la kukusudia

Mchumba wa zamani wa rubani aliyedondosha ndege kusudi katika milima ya Ufaransa ya Alps, ananukuliwa na gazeti moja la Ujerumani akisema kuwa Andreas Lubitz alikuwa akipanga njama kubwa.

Mwanamke huyo, muandalizi katika ndege, ambaye alikutana na rubani huyo kazini mwaka jana 2014, aliliambia gazeti la Bild kwamba rubani Lubitz alisema mara nyingi kwamba atafanya kitu ili kila mtu amkumbuke yeye ni nani.

Alimuelezea kuwa alikuwa mtu aliyekuwa akiteseka kichwani.

Mwandishi wa habari aliyemhoji dada huyo aliiambia BBC kwamba dada huyo alisema Lubitz alikuwa mtu mwema na hodari mbele ya watu, lakini faraghani alikuwa mkali hasa wakizungumzia kazi.

Anasema wakati mwengine anapata jinamizi na anaamka akipiga kelele "ndege inaanguka."

Anasema Lubitz alikasirika alipotambua hivi karibuni kwamba alikuwa hawezi kutimiza ndoto yake ya kuwa rubani kamili, kwa sababu ya ugonjwa wa akili.

Baada ya uhusiano wa siri baina yao kwa miezi mitano, dada huyo alijitenga na Lubitz kwa sababu ya hasira zake.
Eneo lililotokea ajali ya ndege ya Germanwings kwenye milima ya French Alps, Machi 24, 2015 na kwamba hakuna mtu yeyote aliyenusurika kati ya abiria 150 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo aina ya Airbus A320 .
Ndege ya Germanwings Airbus A320 iliyosajiliwa kwa D-AIPX ilivyoonekana kwenye uwanja wa ndege wa Berlin, March 29, 2014.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad