![]() |
|
Wanafunzi wa mwaka wa kwanza Diploma,Higher Diploma na Certificate
tawi la Ngara,Mkoani Kagera.
DAR ES SALAAM INSTITUTE OF JOURNALISM AND MASS
COMMUNICATION-NGARA BRANCH.
(Proprietor of TUPOSE
Polytechnics Limited)
P.O. Box 12893, DAR-ES SALAAM.
TANZANIA.
Tel: +2558421849 / +255689594150/ +255713 112 84
Website:
www.dijmc.ac.tz
NGARA- BRANCH
Baada ya serikari ya
Tanzania kuja na mkakati wa kuanzisha shule za sekondari katika kila kata
ilioanza mapema mwaka2006.
Mkakati huu ulifanikiwa ambapo shule za sekondari za
kata ziliongezeka kila mwaka mpaka sasa 2015.
Lakini katika kuanzisha shule hizi
mambo makuu manne yaliachwa nyuma ikiwa ni:
Kutoweka mazingira rafiki ya shule hizi kwa
mwanafunzi.
Kutokua na walimu wa kutosha na wenye
taaluma sahihi ya kufundisha watoto
Kutotoa vifaa vya kujisomea na kufundishia
kama vitabu vya ziada na kiada.
Kutoweka mpango wa maabara ili kujifunza
kwa vitendo hasa masomo ya sayansi.
Baada ya vitu hivyo
kuachwa nyuma na ni vitu vya msingi sana kwa mstakabari wa elimu bora,amabapo
imefanya idadi kubwa ya wanafunzi wengi wanaohitimu kuishia kupata alama ndogo
baada ya mambo ya msingi sana kama yalivyotajwa hapo juuu kutotolewa kwa ustadi
unaotakiwa.
Kibaya Zaidi serikali
haikuandaa mpango wa kuwasaidia hawa vijana wetu waliokosa elimu bora kwamba
hatima yao ni ipi baada ya masomo yao,kitu kinacho sababisha idadi kubwa ya
vijana kukaa vijiweni maana hawajaandaliwa katika mazingira ya kujiendeleza.
Lakini pia kuna hii
sharia ya wafanyakazi wa serikaki,kama mtu ni mtumishi wa serikari hapaswi
kujiendeleza kabla ya kua kazini kwa mda usiopungua miaka mitatu.
Hii kiukweli
haingii akilini kwani kujiendeleza kitaaluma ni sehemu ya kuongeza ufanisi
kazini na hata maisha binafsi ya mfanyakazi.Jambo hili limewakosesha vijana
wengi wanaofanya kazi katika asasi za kiserikali na wale wanaofanya kazi katika
asasi zisizo za serikali kujiendeleza kitaaruma.
Baada ya utafiti
uliofanywa na Mr.Eliud Amoni Ruzige kipindi nikiwa anachukua shahada yangu ya
uhasibu na Fedha katika chuo kikuuu cha Mtakatifu Augustino-Mwanza mwaka 2014.
Utafiti
huu uliibuka na mapendekezo ya kuanzisha vyuo mbalimbali visivyo na masharti
magumu ili kuwasaidia vijana wengi wanao maliza kidato cha nne na sita pamoja
na wale wanaofanya kazi katika asasi za kiserikali na zisizo za kiserkali
kujiendeleza katika maeneo yao ya kufanyia kazi ili kuleta tija na ufanisi
kazini na katika maisha yao binafsi.
Ndipo nilifanikiwa
kushawishi mkurugenzi wa chuo cha DAR ES
SALAAM INSTITUTE OF JOURNALISM AND MASS COMMUNICATION kufungua tawi KATIKA
WILAYA YA NGARA.ambapo imesaidia vijana wengi wa wilaya hii ilioachwa nyuma
kielimu tangu uhuru mpaka sasa haijawahi kua na chuo chochote cha kusaidia
wanajamiii achilia mbali chuo cha ufundi Lemera ambapo pia hakija kidhi
mahitaji kwa viwango vyake.
Mpaka sasa tumeshafungua
tawi la chuo, eneo la Afriline Kogifa-Ngara barabara ya Nyamiaga mkabara na
ikulu ndogo ya wilaya.
Hapa tunatoa program
mbalimbali katika ngazi ya Cheti(Certificate) ngazi ya stashahada (Diploma) pamoja
na Stashahada ya juu(Higher Diploma) katika kozi zifuatazo:-
Ø Accountancy and Finance( Uhasibu na fedha )
Ø Procurement and Logistic(Ugavi na manunuzi)
Ø Law
(Sheria)
Ø Information Communication Technology-ICT(Mawasiliano
na tekinologia)
Ø Journalism and Mass
communication(mawasiliano ya uma na utangazaji)
Ø Community Development(Maendeleo ya jamii)
Ø Business Administration (Usimamizi na
Uratibu wa Biashara)
Ø Record management(Utunzaji wa takwimu na
kumbukumbu)
Tumeanza masomo rasmi tarehe.12/01/2015,ambapo mpaka sasa
tuna wanafunzi 34 Wanaendelea na masomo darasani.
Binafsi naomba kutoa wito kwa wakazi wa ngara na maeneo
jirani kama wilaya jirani za karagwe,Bimlo,Kakonko,Kibondo nan chi jirani kama
Rwanda na Burundi kua hii ni fursa pakee ya kupata elimu kwa vigezo
nafuu,Gharama nafuu,na karibu kabisa.
TUTAANZA USAJILI WA PILI (INTAKE TWO) TAREHE.2//2015.
Tunawakalibisha
wale wote waliomaliza kidato cha nne,wafanyakazi wa asasi za serikari na zisizo
za kiserikari wanaohitaji kuiendeleza.
Hostel zinapatikana kwa
gharama nafuu sana kwa wale wanaotoka mbali na chuo kilipo.
Mimi naamini mtu anapo pata taaruma Fulani ama ya
udaktari,uhasibu,ugavi na mengine ni fursa pekee ya kumuwezesha kupata ajira
rasmi lakini pia inaweza kumufanya kuweza kujiajili na hatimae kutengeneza
ajira kwa watu wengine ikiwa ni mkakati wa kupunguza ajira katika TAIFA letu
pendwa la Tanzania.
Nawakalibisheni sana,kama unahitaji maelekezo yeyote juu
ya chuo chetu.
Fika Afriline Kogifa eneo tawi la chuo kilipo au
wasiliana nasi kwa nambari zifuatazo
0758421849, 0689594150 au 0756258273
nasi tutakujibu kwa
wakati.
IMETOLEWA
NA:-
Mr. ELIUD RUZIGE
BRANCH
CORDINATOR DAR ES SALAAM INSTITUTE OF
JOURNALISM AND MASS COMMUNICATION-NGARA BRANCH.
UNGANANASI KATIKA FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Monday, February 09, 2015
Home
HABARI
SOMA TANGAZO HILI:-Ni Muhimu sana kwa Mnaopenda Kusoma Elimu ya Juu wilayani Ngara,mkoani Kagera.
SOMA TANGAZO HILI:-Ni Muhimu sana kwa Mnaopenda Kusoma Elimu ya Juu wilayani Ngara,mkoani Kagera.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment