|
Naibu Katibu
mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Upande wa Zanzibar,Bw.
Salum Mwalimu akivishwa skafu na kamanda wa skauti Nelson Felix alipokuwa
amewasili Jana Februari 08,2015,Jimbo la Muleba Kusini mkoani Kagera
kuhutubia Wananchi wa jimbo hilo..Picha/Habari Na:-Shaaban Ndyamukama.
Wananchi
wilayani Muleba mkoani Kagera wameshauriwa kuhakikisha wanajiamini na
kusimamia rasilimali zao zikiwemo zinazotoka ndani ya ziwa victoria ili waweze
kuzitumia kwa manufaa yao na kizazi kijacho.
Katibu wa
Baraza la Wazee (CHADEMA) ngazi ya Taifa ,Bw.Rodrick Tutembeka amesema hayo
jana Februari 08,2015, katika mkutano wa Hadhara uliofanyika Katika Jimbo
la Muleba Kusini na kudai kuwa baadhi ya rasilimali kama ardhi zinaporwa
na wenye nyadhifa Serikalini.
Bw.Rutembeka
amesema kuwa kinachohitajika ni kupaza sauti zao kudai haki ya umilikaji wa
ardhi kwa usawa na kuwekeza ndani ya ziwa ili kujipanua kiuchumi kwa kuvua
samaki na dagaa na kuuziana wao kwa wao na kujiongezea mapato.
Amesema kuwa
jambo lingine ni kuishinikiza serikali kupitia viongozi waadilifu wa kisiasa na
wenye utashi wa kutetea haki na maslahi ya taifa kutumia ziwa victoria
kusambaza huduma ya maji vijijini ili kuondoa usumbufu uliopo.
Aliongeza
kuwa wilaya ya Muleba inazo rasilimali ambazo viongozi waadilifu wakipatikana
kupitia vyama bora na imara vya kisiasa umaskini kwa watanzania unaweza kuwa
ndoto kwani wanaweza kuelimishwa kujikwamua kiuchumi.
|
No comments:
Post a Comment