PICHA / HABARI:-Huyu ni mtoto wa miaka miwili aliyetoka salama kwenye hii ajali ya ndege. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 05, 2015

PICHA / HABARI:-Huyu ni mtoto wa miaka miwili aliyetoka salama kwenye hii ajali ya ndege.

Taswira kutoka eneo la ajali hiyo. ..Mtoto wa kiume wa miaka miwili amenusurika kufa katika ajali ya ndege iliyoua watu 31 huko Taiwani baada ya kukosa mwelekeo na kuangukia mtoni katika mji wa Taipei.

 Ndege inayoimilikiwa na Shirika la Ndege la Taiwan, la TransAsia imepata ajali na kuangukia kwenye mto katika mji mkuu, Taipei na Mpaka sasa tayari watu 15 wameokolewa kutoka kwenye ndege hiyo huku wengine 12 wakiwa hawajulikani walipo.

Waokoaji wakimchukua mtoto huyo baada ya kumwokoa kutoka kwenye ndege hiyo.
Vyombo vya habari vya Taiwan vimesema Mtoto huyo pichani alikutwa akilia nje ya ndege hiyo na kuchukuliwa na waokoaji kisha kumkimbiza hospitali kwa uchunguzi zaidi.

Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 58 ilipita karibu na magari na kudondoka mtoni muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Songdshan, Taipei kuelekea uwanja wa ndege wa Kinmen nje ya Taiwan huku  chanzo cha ajali  kikiwa bado hakijajulikana.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad