LIGI YA MABINGWA:- Azam FC yaizima El Merreikh..'' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 16, 2015

LIGI YA MABINGWA:- Azam FC yaizima El Merreikh..''

Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu akishangilia na wenzake baada ya kuifungia bao la kwanza wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El Merreikh ya Sudan jana Februari 15,2015 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

 Mabingwa wa Tanzania Bara 2013/2014, Azam FC wameanza kwa kishindo Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa El Merreikh kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mshambuliaji Didier Kavumbagu alifungia Azam FC bao la kuongoza dakika ya 9, kabla ya Nahodha John Bocco aliyeingia akitokea benchi kupachika bao la pili kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara na kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele kabla ya mchezo wa marudiano.

Ushindi huo wa Azam FC umekuja ikiwa ni siku moja baada ya wawakilishi wengine wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho, Yanga SC kuichapa BDF XI kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi Februari 14,2015.

UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad