|
Mamlaka ya
Chakula na Dawa Tanzania,TFDA imefuta usajili wa aina tano za dawa baada ya
kubaini kuwa zina madhara na hazifai kwa matumizi ya Binadamu.
TFDA
imefikia hatua hiyo baada ya dawa hizo kubainika kuwa na viambata
vinavyosababisha maradhi sugu ikiwemo kiharusi, na wakati mwingine kusababisha
vifo na kuamuru aina tano za dawa za binadamu ziondolewe sokoni na vituo vyote
vya kutolea huduma za afya nchini kote mara moja .
Aina tano za
dawa zinazotajwa kufutiwa usajili na kuzuia uingizwaji kuwa ni pamoja na dawa
ya kutibu Fungus ya vidonge na Kasuli aina ya Ketoconazole, dawa
ya kutibu Malaria ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine (Monotherapy), dawa
za kutibu mafua na kikohozi za maji, vidonge na Kapsuli zenye kiambato hai aina
ya Phenylpropanlo Amine, dawa ya kuua bakteria ya sindano aina ya
Chloramphenicol Sodium Succinate inayotengenezwa na kiwanda cha
Lincoln Pharmaceuticals Ltd, India na dawa ya Kuua bakteria
ya maji na kapsuli aina ya Cloxacillin.
Mkurugenzi
Mkuu Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bw.Hiit Sillo amesema hatua hiyo
imefikiwa baada ya uchunguzi wa kitaalam wa muda mrefu kwa kutumia mifumo ya
ufuatiliaji wa usalama na ubora wa dawa ambao pia unafanya kazi kwa kutumia
mtandao wa kimataifa kwa ushirikiano wa shirika la afya duniani WHO.
Aidha TFDA
imefanya mabadiliko ya matumizi ya dawa ya maralia ya SP kutumika kama kinga ya
maralia kwa wanawake wajawazito tu na kuagiza watengenezaji kubadili machapisho
na vifungashio vyake mara moja.
Mkurugenzi
wa Dawa TFDA, Mitanga Fimbo, pamoja na kufafanua athari zake amewataka
watoa huduma nchini kote kuondoa dawa hizo na kuziteketeza mara moja kabla ya
kuanza kwa msako.
|
No comments:
Post a Comment