AFCON 2015:-Matukio ya Picha Ivory Coast walivyofurahia Jana Februari 04,2015 kutinga Fainali huku Ghana na Equitorial Guinea leo Saa 4 Usiku. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 05, 2015

AFCON 2015:-Matukio ya Picha Ivory Coast walivyofurahia Jana Februari 04,2015 kutinga Fainali huku Ghana na Equitorial Guinea leo Saa 4 Usiku.

Mashabiki wa Kikosi cha Timu ya Taifa ya Ivory Coast,ambacho kimefanikiwa kuwa Timu ya kwanza kutinga Fainali ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, baada ya Jana Februari 04,2015,Usiku huko Estadio de Bata, Mjini Bata, Nchini Equatorial Guinea, kuichapa Congo DR Bao 3-1.


Wafungaji wa mabao ya Ivory Coast walikuwa Yaya 21', Gervinho 41', Kanon 68' huku bao la DR Congo likifungwa na Mbokani 24' kwa penati.

Kwa matokeo hayo, Ivory Coast wanasubiri mshindi wa mechi ya leo Februari 05,2015,saa Nne usiku kati ya Ghana na wenyeji Equitorial Guinea kucheza naye katika fainali itakayopigwa Februari 8, mwaka huu.

DR Congo wanasubiri atakayefungwa kwenye mechi ya hiyo ili wacheze naye Februari 7, mwaka huu kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya tatu na ya nne.

Kipa wa DRC, Kidiaba akijaribu kuokoa mpira wa kichwa ulipigwa na Gervinho bila mafanikio. Hata hivyo mpira huo uliokolewa na mchezaji wa DRC ukielekea nyavuni.



UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad