WAFAHAMU MAWAZIRI NANE WAPYA:-Ni walioteuliwa na Kuapishwa Januari 24,2015 na Rais Kikwete wa Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 25, 2015

WAFAHAMU MAWAZIRI NANE WAPYA:-Ni walioteuliwa na Kuapishwa Januari 24,2015 na Rais Kikwete wa Tanzania.

Hapo Jana jumamosi Januari 24,2015,Majira ya Mchana huenda ikawa moja ya siku ambazo zitaingia kwenye Mazungumzo Makubwa katika anga za siasa TANZANIA 2014/2015 ambapo January 24 2015 ,kulikuwa na taarifa za kujiuzulu kwa Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospiter Muhongo.

Kubwa Jingine kwenye upande huo huo ni Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano.

Tangazo hilo lilifanywa na Katibu Mkuu katika Ikulu ya Rais Balozi Ombeni Sefue.

Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhifa wa Waziri wa Nishati na Madini wa Profesa Muhongo ambaye amejiuzulu pamoja na wadhifa wa Waziri wa ardhi ambao uliawachwa wazi baada ya kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.

Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu pia kujiuzulu.
Waziri wa Nishati na Madini mpya, Bw.George Simbachawene.

Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe.

Waziri wa Mahusiano na Uratibu, Bi.Mary Nagu.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Bw.Wiliam Lukuvi.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Bw.Steven Wassira.

Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Bw.Christopher Chiza.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Bw.Steven Masele.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi, Bi.Angellah Kairuki.

Naibu Waziri Katiba na Sheria,Bi.Ummy Mwalimu.

Bi.Anne Kilango Malechela mbunge wa mbunge wa jimbo la Same Masharikinaye hii ni mara yake ya kwanza kuingia serikalini baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu

Charles Mwaijage - Pichani ni  Mbunge wa Muleba Kaskazini CCM,Bw. Charles Mwijage ambaye ameteuliwa kwa mara ya kwanza kushika nafasi ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini.


Mawaziri.

Bw.George Simbachawene – Waziri wa Nishati na Madini

Bi.Mary Nagu - Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais- Mahusiano na Uratibu

Bw.Christopher Chiza - Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji

Bw.Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Bw.William Lukuvi - Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi

Bw.Steven Wasira - Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

Bw.Samuel Sitta - Waziri wa Uchukuzi

Bi.Jenista Muhagama - Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge

Manaibu Waziri.

Bw.Stephen Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais- Muungano

Bi.Angela Kairuki - Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi

Bi.Ummy Mwalimu - Naibu Waziri wa Katiba na Sheria

Bi.Anne Kilango - Naibu Waziri wa Elimu 

Bw.Charles Mwaijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini. 



UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad