PAMOJA TUNAWAKILISHA:-Yaliyojiri Januari 24,2015 wakati Wafanyakazi wa Radio Kwizera FM walipojumuika pamoja katika Sherehe la kufunga na Kufungua Mwaka 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 25, 2015

PAMOJA TUNAWAKILISHA:-Yaliyojiri Januari 24,2015 wakati Wafanyakazi wa Radio Kwizera FM walipojumuika pamoja katika Sherehe la kufunga na Kufungua Mwaka 2015.


Watumishi wa Radio Kwizera Mkoani Kagera, Kigoma na DRC wakiwa  katika picha ya Pamoja na  Mkurugenzi wa Radio Kwizera, Fr Damas Missanga wa pili kutoka kushoto,Kaimu Mkurugenzi Br. Deus, HRO Bw.Donatus Baltazar na Mkuu wa Uzalishaji Vipindi Bi Joyce Ngallawa.


 Jana Januari 24,2015, Wafanyakazi wa Radio Kwizera FM makao makuu Ngara 97.9 FM na wale wa Vituo vya Kibondo 93.6 FM,Kasulu na Kigoma 94.2 FM pamoja na Mashariki mwa DRC walikutana pamoja katika Hafla ya Kuuaga na Kuukaribisha Mwaka Mpya 2015 (Together Party) iliyofanyika katika Viwanja vya GARDEN mjini Benaco,wilayani Ngara mkoani Kagera.


Toka Kushoto ni Babu Ismail toka Kasulu,Hamis Mkama toka Ngara wakiwakilisha Idara ya Usafiri sambamba na Rehema Ruhotola .

Toka Kushoto ni Albert Kavano toka Mwanza,Lokendo toka DRC wakiwa na Br Deus wakati wa Hafla hiyo ya Wafanyakazi wa Radio Kwizera FM.

Toka Kushoto ni Yohana Bitta Kaimu Fundi Mkuu sambamba na Juventusi Juvinary  kutoka Biharamulo katika pozi.
Toka Kushoto ni Elasimus Luziro kutoka Kigoma  katika pozi na Lubanga Nathanael ambaye ni Kaimu Production Officer.


Toka Kushoto ni Bi.Anna Matenga Team Leader kituo cha Kibondo katika pozi na Maalim Shaaban Ndyamukama.

Hii ya Babu Ismail kwa mbele daaaaa...ni kali zaidi yaaa.....sambamba na Fr.Sixmund Nyabenda toka kushoto,Fadhil Kijanjali,Chief Editor Seif Omary Upupu na Kosta Kasisi katika amsha amsha za sherehe.

Toka Kushoto ni Brother Deus na CEO wa Makonda Blog na Mkuu wa Idara ya Studio Mwana wa Makonda  katika pozi .


Toka Kushoto ni Omary Mbwambo Team Leader kituo cha Kasulu,mkoani Kigoma katika pozi na Afisa Masoko Smith Swai.

...............Kitengo cha Nyama choma kikiwajibika ......


Pamoja na Halfa hiyo kuambatana na Burudani ya Muziki,Kuonesha Vipaji vya Uimbaji,Uchezaji Muziki ,Kucheza Mpira , Mkurugenzi wa Radio Kwizera, Fr Damas Missanga amewawataka Wanahabari wa Kituo hicho   kuthamini kwanza usalama wa maisha yao wakati wa kufatilia habari /matukio  kwani wanaweza kuwa chambo cha  kupoteza maisha yao.

Katika matukio makubwa ya kusisimua kisiasa mwaka huu 2015, Fr Damas Missanga kawataka wanahabari kuhakikisha wanaripoti habari zisizo za ushabiki wala uchochezi  na kuwapa nafasi wanaolalamikiwa kutoa maoni yao bila kutumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao binafsi sambamba na kufanya uchunguzi wa kina na kuhoji mamlaka husika ili kila mmoja kupata haki yake ili kukuza demokrasia na utawala bora.

Kuanzia Mwezi februari mwaka huu , Kituo cha Radio Kwizera kinatarajia kupanua huduma zake za matangazo katika Miji ya Bukoba,Kahama na Mwanza  ambapo kwa sasa pia kikisikika kupitia njia ya mtandao kwa tovuti yetu ya www.radiokwizera.com na www.radiostationstz.com.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad