LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Ilichokifanya Yanga SC January 24, 2015 Morogoro ….Leo Simba SC na Azam FC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 25, 2015

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Ilichokifanya Yanga SC January 24, 2015 Morogoro ….Leo Simba SC na Azam FC.

Bao pekee la mshambuliaji Danny Mrwanda limeizindua Yanga SC na kuipa ushindi wa tano msimu huu katika mechi pekee ya Jana January 24, 2015 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Polisi Moro iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

 Mrwanda alifunga bao hilo dakika ya 42 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Tony Kavishe wa Polisi Moro kufuatia shuti kali la krosi ya beki wa pembeni kulia Juma Abdul.

Hilo ni bao la tano kwa Mrwanda baada ya kufunga pia mabao manne katika mechi saba alizokichezea kikosi cha Kocha Adolf Richard cha Polisi Moro mwanzoni mwa msimu huu kabla ya kujiunga na Yanga SC dirisha dogo.

Mrwanda, ambaye hakufunga katika mechi mbili zilizopita ambazpo Yanga SC ilitoka sare ya 2-2 dhidi ya Azam FC na 0-0 dhidi ya Ruvu Shooting, sasa yuko sawa na Ame Ally Amour wa Mtibwa Sugar FC na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar wenye mabao matano pia.

Kwa ushindi huo, Yanga SC ambayo imeshinda mechi nyingine nne msimu huu 2014/2015 dhidi ya Tanzania Prisons, JKT Ruvu, Stand United na Mgambo ikishikwa kwa sare na Simba SC, Azam FC na Ruvu Shooting Stars na kufungwa na wakatamiwa Mtibwa Sugar FC na Kagera Sugar FC, imefikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi 10.

Kikosi hicho cha Pluijm sasa kiko kimepanda hadi nafasi ya pili ya msimamo wa VPL kikizidiwa pointi mbili na vinara Azam FC ambao pia wamecheza mechi 10 na kesho watakipiga dhidi ya Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ligi itaendelea leo Jumapili kwa Mechi 6 na Bigi Mechi ni Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kati ya Mabingwa Azam FC na Simba.

Mechi nyingine za Jumapili ni pamoja na ile ya Kagera Sugar na Ndanda FC ambayo itachezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Jijini Mwanza kutokana na Kaitaba Stadium kufanyiwa ukarabati.

RATIBA.

Jumapili Januari 25,2015.

Azam FC v Simba 

Kagera Sugar v Ndanda FC [CCM Kirumba, Mwanza]

Stand United v Coastal Union

Mbeya City v Tanzania Prisons

Ruvu Shooting v Mtibwa Sugar

JKT Ruvu v Mgambo JKT

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad