|
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw John Nshimilimana (Pichani mwenye miwani) akitazama ramani inayoonesha taswira ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera hivi karibuni akiwa na Madiwani wenzake wakati wa ziara ya kukagua Maendeleo wilayani Ngara.
Halmashauri
ya wilaya ya Ngara Mkoani Kagera huenda ikasimamisha shughuli zake za
maendeleo, kutokana na uhaba wa fedha za maendeleo zinazotegemea ruzuku kutoka
serikalini na vyanzo vyake vya mapato.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw John Nshimilimana, amesema hayo wakati
akiongea na RADIO KWIZERA FM, ambapo amesema kuwa kutokana na uhaba huo
wameshindwa kufanya vikao halali kutokana na ukosefu wa posho.
Bw Nshimilimana
amesema uhaba huo ulianza mwezi Octoba mwaka jana,2014 ambapo Halmashauri hiyo ilitegemea
kupokea fedha za ruzuku Shilingi bilioni 2.5 lakini hadi sasa haijapokea fedha
hizo hali inayosababisha miradi ya maendeleo kusimama.
Amesema
baadhi ya miradi iliyokosa fedha na kusimama ni pamoja na maji, ukarabati wa
barabara za vijiji wilayani humo, huku idara ya afya ikishindwa kufika katika
vituo vya kutolea huduma kwa kukosa mafuta ya kusafiria.
Chanzo:-Radio Kwizera/Habari.
|
No comments:
Post a Comment