Mtandao wa
kijamii wa WhatsApp unawabana watu wanaotumia huduma hio kupitia programu
bandia na ambayo haijaidhinishwa ya Android kwa muda wa saa 24.
WhatsApp
ambayo inamilikiwa na Facebook, ilisema kuwa imechukua hatua dhidi ya watumiaji
wa huduma ya WhatsApp Plus kwa sababu ya wasiwasi kwamba programu hiiyo huenda
iksababisha kuvuja kwa taarifa za siri za watumiaji wa WhatsApp.
Programu hio
bandia na isio rasmi ya Android inawezesha watumiaji wa WhatsApp Plus kupamba
mawasiliano yao wanavyotaka.
Wataalamu
wanasema kwamba watumiaji wa Android wanapaswa kuwa makini na kutahadhari
kuhusu wanavyodownload programu flani au 'Apps'.
Mtandao wa
WhatsApp ulisema hivi karibuni kwamba ina watumiaji milioni 700 wanaotuma ujumbe
bilioni 30 kila siku. Kwa sasa inatoza dola 0.99 kwa watumiaji wake wanaotumia
huduma ya WhatsApp Plus kila mwaka.
''Lengo letu
ni kuhakikisha kwamba huduma ya WhatsApp ni ya kasi kwa wanaoitumia, hilo ndio
jambo muhimu sana kwetu,'' alisema msemaji wa kampuni hio.
''Watu
wengine wamebuni progarmu ambazo bado hazijaidhinishwa na sasa wanazitumia na
WhatsApp , kitu ambacho kinaweza kusababisha kupotea kwa ujumbe au baadhi ya
taarifa kuvujishwa. ''
''Bila shaka
jambo hili linakwenda kinyume na malengo yetu ya kutoa huduma kwa wateja wetu.
Kuanzia leo tutaanza kuchukua hatua kali dhidi ya wanaotumia programu ambazo
hazijaithinishwa ili kuweza kutumia programu zetu na pia kuwatahadharisha
wanaozitumia programu hizo''.
Kulingana na
moja ya maduka ya kuuza programu za kwenye mitandao, programu ya WhatsApp Plus
yenyewe ilikuwa imekuwa dowloaded mara milioni 35
|
No comments:
Post a Comment