LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Matokeo ya Leo Januari 18,2015 huku Mtibwa Sugar wakiwatoa kileleni mwa msimamo Mabingwa watetezi wa Ligi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 18, 2015

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Matokeo ya Leo Januari 18,2015 huku Mtibwa Sugar wakiwatoa kileleni mwa msimamo Mabingwa watetezi wa Ligi.

Mabingwa mara mbili wa Tanzania, 1999 na 2000, Mtibwa Sugar wamewatoa kileleni mwa msimamo Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, Azam FC baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na wenyeji JKT Ruvu katika mchezo uliomalizika jioni ya leo Januari 18,2015,kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es salaam.

Azam walirejea kileleni jana Januari 17,2015 baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand United uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga,  ambapo walifikisha pointi 17 na magoli 11 ya kufunga kufuatia kushuka dimbani mara 9.

Kutokana na Mtibwa Sugar kuvuna pointi moja, wamefikisha pointi 17 sawa na Azam FC, lakini wamewazidi wakali hao wa Chamazi kwa magoli ya kufunga kwani sasa wametikisa nyavu mara 12 katika mechi 9 walizokipiga.

JKT Ruvu nao wamefikisha pointi 17 katika nafasi ya tatu kutokana na kuwa na magoli 11 katika mechi 11 walizocheza.

JKT Ruvu walitangulia kupata Bao Dakika ya 7 Mfungaji akiwa Samuel Kamuntu na Amer Ali kuisawazishia Mtibwa katika Dakika ya 37.

Mechi nyingine ya Ligi kuu imepigwa uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga ambapo Wagosi wa Kaya, Coastal Union wametoka suluhu (0-0) dhidi ya Polisi Morogoro.
Kwa matokeo hayo Coastal Union wamefikisha pointi 12 wakati Polisi Moro wamefikisha pointi 15.

Ligi hii itaendelea hapo Jumanne huko Mwanza kwa Mabingwa Azam FC kuwavaa Kagera Sugar ambao sasa wanatumia CCM Kirumba kama Uwanja wa Nyumbani baada ya Kaitaba huko Bukoba kufungwa kwa ukarabati.

RATIBA.

Jumanne Januari 20,2015

Kagera Sugar na Azam FC (Mwanza)

Jumamosi Januari 24,2015

Azam FC v Simba 

Kagera Sugar v Ndanda FC

Stand United v Coastal Union

Polisi Morogoro v Yanga

Mbeya City v Tanzania Prisons

Ruvu Shooting v Mtibwa Sugar

Jumapili Januari 25,2015.

JKT Ruvu v Mgambo JKT

MSIMAMO.

NA
TIMU
P
W
D
L
F
 A
 
GD
PTS
1
Mtibwa Sugar
9
4
5
0
12
5
 
7
17
2
Azam FC
9
5
2
2
11
6
 
5
17
3
JKT Ruvu
11
5
2
4
11
10
 
1
17
4
Yanga
9
4
3
2
11
7
 
4
15
5
Polisi Moro
11
3
6
2
9
8
 
1
15
6
Kagera Sugar
10
3
5
2
7
5
 
2
14
7
Coastal Union
10
3
4
3
9
8
 
1
13
8
Mgambo JKT
10
4
1
5
5
9
 
-4
13
9
Simba
9
2
6
1
9
7
 
2
12
10
Ruvu Shooting
11
3
3
5
5
8
 
-3
12
11
Mbeya City
9
3
2
4
4
6
 
-2
11
12
Stand United
11
2
5
4
7
13
 
-6
11
13
Ndanda FC
11
3
1
7
10
16
 
-6
10
14
Tanzania Prisons
10
1
5
4
6
8
 
-2
8

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad