EPL 2014/2015:-Picha 7 za Manchester City ikifungwa 0 - 2 na Arsenal: ni Santi Cazorla's na Olivier Giroud's wangara Etihad Stadium. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 18, 2015

EPL 2014/2015:-Picha 7 za Manchester City ikifungwa 0 - 2 na Arsenal: ni Santi Cazorla's na Olivier Giroud's wangara Etihad Stadium.

Leo hii Januari 18,2015, Arsenal wametoka Vidume baada ya kuwacharaza Mabingwa wa Uingereza  Manchester City 2-0 Uwanjani Etihad Jijini Manchester na wao kujiletea matumaini ya kufuzu 4 Bora huku wakiwaacha Man City wakiwa Pointi 5 nyuma ya Vinara Chelsea kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Uingereza msimu wa mwaka 2014/2015.

Ushindi huu umewafanya Arsenal wawe Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Man United walio Nafasi ya 4, Pointi 3 nyuma ya Timu ya 3 - Southampton, Pointi 7 nyuma ya Man City na Pointi 12 nyuma ya Vinara Chelsea.

Kwa City hili ni pigo kubwa hasa baada ya kuwa na wimbi la Mechi 12 bila kufungwa na hasa ukizingatia Mechi yao inayofuata ya Ligi ni ya Ugenini hapo Januari 31,2015  huko Stamford Bridge dhidi ya Chelsea.



Ushindi huu wa Arsenal ulianza kwa Penati laini aliyotoa Refa Mike Dean baada ya kuamua Vincent Kompany amemchezea Faulo Nacho Monreal na Santi Cazorla kufunga Penati hiyo katika Dakika ya 24.

Arsenal walifunga Bao lao la Pili Dakika ya 66 baada ya Frikiki ya Cazorla kuunganishwa kwa Kichwa na Olivier Giroud.


Nao West Ham wamepanda hadi kufikia Nafasi ya 7 kwenye Ligi Kuu wakiwa Pointi 4 nyuma toka zile Nafasi 4 za juu baada ya Leo Januari 18,2015 kuitwanga Hull City Bao 3-0 walipokuwa kwao Upton Park.

Bao zote za West Ham zilifungwa Kipindi cha Pili na Andy Carroll, Dakika ya 49, baada ya Kipa Allan McGregor kutema Shuti la Enner Valencia, kisha Dakika ya 69 Morgan Amalfitano alifunga Bao la Pili na Stewart Downing kupachika Bao la 3 Dakika ya 72 baada ya Kiungo wa West Ham Alex Song kuichambua Difensi ya Hull City.

Matokeo haya yameifanya Hull, ambayo ina Majeruhi wengi, kushika Nafasi ya 18 wakiwa moja ya Timu 3 za mkiani ambazo ziko eneo hatari la kushuka Daraja.
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad