LIGI KUU VODACOM 2014/2015:- Matokeo ya Mechi za leo January 17,2015 Azam FC, Simba SC na Mbeya City safi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 17, 2015

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:- Matokeo ya Mechi za leo January 17,2015 Azam FC, Simba SC na Mbeya City safi.

Mpira ukigonga mwamba kwenye lango la Ruvu Shooting, kufuatia kona ya Andrey Coitinho (hayupo pichani)  kuunganishwa kwa kichwa na Simon Msuva Kwenye mchezo wa Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara 2014/2015 leo Januari 17.

  Yanga SC imepata sare ya pili mfululizo baada ya kumaliza dakika 90 dhidi ya Ruvu Shooting bila bao.


Sare hiyo inakuwa ni ya pili kwa Kocha Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi ambaye amerejea kuinoa Yanga.

Katika mechi hiyo ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Yanga ilipoteza zaidi ya nafasi tatu za kufunga kupitia Simon Msuva, Amissi Tambwe na Andrey Couinho.
Kocha Goran Kopunovic ameanza Ligi Kuu Bara vizuri baada ya kuiwezesha Simba SC kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.

Simba SC imeshinda mechi hiyo ikiwa ugenini leo Januari 17,2015 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Vijana hao wa Msimbazi walifunga bao kila kipindi wakianza kupitia kwa Danny Sserunkuma aliyeonekana kufanya vizuri katika mechi hiyo ambapo Kipindi cha pili, Simba SC ilikianza vizuri na harakaharaka ilifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Elius Maguli.

Huu ni ushindi wa pili kwa Simba SC  tokea ilipoifunga Ruvu Shooting mwishoni mwa mwaka jana 2014 ,ukiwa ni ushindi pekee chini ya Patrick Phiri halafu ikatoka sare mechi sita na kupoteza moja dhidi ya Kagera Sugar.

Huko Kambarage,Mkoani  Shinyanga, Azam FC wameifunga Stand United Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 43 la Frank Domayo na kukaa kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 1 mbele ya Mtibwa Sugar ambao wanacheza Jumapili januari 18,2015 Ugenini na JKT Ruvu.

Huko CCM Kirumba, Mwanza, Mbeya City wameifunga Kagera Sugar, wanaotumia Uwanja huo kwa Mechi za Nyumbani baada Kaitaba kufungwa kwa ukarabati, Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 80 la Peter Mapunda.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

RATIBA VPL.

Jumapili Januari 18,2015.

JKT Ruvu v Mtibwa Sugar

Coastal Union v Polisi Morogoro

MSIMAMO.

NA
TIMU
P
W
D
L
F
 A
GD
PTS
1
Azam FC
9
5
2
2
11
6
5
17
2
Mtibwa Sugar
8
4
4
0
11
4
7
16
3
JKT Ruvu
10
5
1
4
10
9
1
16
4
Yanga
9
4
3
2
11
7
4
15
5
Kagera Sugar
10
3
5
2
7
5
2
14
6
Polisi Moro
10
3
5
2
9
8
1
14
7
Simba
9
2
6
1
9
7
2
12
8
Coastal Union
9
3
3
3
9
8
1
12
9
Ruvu Shooting
11
3
3
5
5
8
-3
12
10
Mgambo JKT
9
4
0
5
5
9
-4
12
11
Mbeya City
9
3
2
4
4
6
-2
11
12
Stand United
11
2
5
4
7
13
-6
11
13
Ndanda FC
11
3
1
7
10
16
-6
10
14
Tanzania Prisons
9
1
4
4
6
8
-2
7

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad