ZIARA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MKOANI TABORA:- Akerwa na kutotumika kwa umeme wa Kontena. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 17, 2015

ZIARA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MKOANI TABORA:- Akerwa na kutotumika kwa umeme wa Kontena.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa maelekezo kwa uongozi wa kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora kuhakikisha umefanya mkutano na wananchi ili kufanya makubaliano jinsi ya kusimamia mradi wa umeme wa kontena ili wananchi waanze kunufaika mara moja.

Mtaalamu kutoka Kampuni ya Chico – CCC, Luo Xiaoyong (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) juu ya hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika wilaya za Uyui na Urambo mara Waziri alipotembelea eneo palipohifadhiwa vifaa kwa ajili ya kazi hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa maelekezo kwa uongozi wa kampuni ya kusambaza umeme katika wilaya ya Uyui na Mirambo ya Chico – CCC ya China mara baada ya kutembelea eneo palipohifadhiwa vifaa kwa ajili ujenzi wa miundombinu ya umeme katika wilaya za Uyui na Mirambo.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wakazi wa kijiji cha Igalula wilayani Uyui mkoani Tabora. Aliyemshikia mwamvuli ni Katibu wake, Joseph Kumburu. 

WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesikitishwa na mradi wa umeme wa Kontena kwenye kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora kuacha kufanya kazi baada ya kuwaka siku chache kwa kile kilichoelezwa kuwa kukosa maelewano ya wananchi na viongozi kutotunga sheria.

Nimesikitishwa na uongozi wa kijiji hiki kutokuwa na utaratibu mzuri na kuelimisha wananchi mradi huu wa umeme wa kontena ni teknolojia iliyokuja kwa majaribio ambapo ni makontena 14 pekee nchi nzima na hiki kijiji cha Tura kimepata bahati kupata umeme huo mimi naona niondoe mradi huu sababu mmeshindwa kuusimamia vizuri,” alisema Waziri Muhongo.

Hata hivyo Waziri Muhongo aliwauliza wananchi na viongozi wa kijiji kuhusu ufahamu wa mradi huo na wananchi walidai kuwa hawaufahamu.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad