EPL 2014/2015:- 5-0 Zaipa Chelsea point 5 mbele huku Manchester United na Liverpool Safi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 17, 2015

EPL 2014/2015:- 5-0 Zaipa Chelsea point 5 mbele huku Manchester United na Liverpool Safi.

Chelsea, wakicheza leo Januari 17,2015 Ugenini, wamepaa kileleni mwa Ligi Kuu Uingereza wakiwa Pointi 5 mbele ya Mabingwa Watetezi Manchester City baada ya kuitandika Swansea City Bao 5-0.

Chelsea walipata Bao lao la kwanza Sekunde 50 tu tangu Gemu ianze kupitia Oscar, kisha Diego Costa akapiga Bao 2 na Oscar kuongeza jingine na kuifanya Chelsea iwe 4-0 hadi Mapumziko.

Kipindi cha Pili, Andre Schurrle akaipa Chelsea Bao la 5 kuiacha Swansea wawe bila ushindi katika Mechi zao 4 za Ligi.


QPR 0 - 2  MAN UNITED .

Nazo bao 2 za Kipindi cha Pili za wachezaji Marouane Fellaini na James Wilson zimewapa ushindi wa Bao 2-0 Manchester United waliocheza Ugenini Loftus Road na QPR.

Ushindi huu umeifanya Man United warudi Nafasi ya 3 na kuitambuka Southampton ambao baadae Leo wako Ugenini kucheza na Newcastle.

ASTON VILLA 0 - 2 LIVERPOOL .

Bao za Frank Borini na Rickie Lambert zimeipa ushindi Liverpool wa Bao 2-0 walipocheza Ugenini Villa Park na Aston Villa.

RATIBA**Saa za Bongo

Jumapili Januari 18,2015.

1630 West Ham v Hull   
            
1900 Man City v Arsenal   
          
Jumatatu Januari 19,2015.

2300 Everton v West Brom 
                  
MSIMAMO.
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad