KIONGOZI WETU:-Mwigulu Nchemba kuhusu Urais, Escrow, kiongozi wa Upinzani anayemvutia yote hapa (Audio). - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 20, 2015

KIONGOZI WETU:-Mwigulu Nchemba kuhusu Urais, Escrow, kiongozi wa Upinzani anayemvutia yote hapa (Audio).

Kama umepitwa na show ya Mkasi ya Januari 19,2015 usiku, hii ilikuwa ya Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, mengi kayazungumza humu ikiwemo ishu ya kutangaza kugombea URAI, ESCROW, SKAFU YAKE na pia kamtaja kiongozi wa upinzani anayemvutia.

 Ishu ya kutamani kugombea Urais;- “Hata kama ningetamani kwa kiwango gani, kama sitatimiza majukumu haya niliyopewa hakuna mtu atakayeniamini…

Rais wa awamu ya nne ameweka rekodi yake ya kutokulinda wahalifu… Ni Rais huyu huyu aliruhusu Waziri wake Mkuu ajiuzulu, ukiangalia kwenye rekodi ni Mawaziri wengi sana wameondoka. Mimi naamini anachotafuta ni hicho tu kutenda haki…”-hapa alikuwa akizungumzia ishu ya maamuzi ya Rais kuhusu Escrow.
Kuhusiana na ishu ya Wafanyakazi wa TRA waliosababisha hasara ya Kodi, Nchemba alisema; “ haiwezekani mtu anayetakiwa kuwajibika kwa Taifa hili akawa Waziri peke yake, hata aliyesoma kwa kodi ya Watanzania ana wajibu kwa Taifa… 

Kwenye siasa ya vyama vingi tunataka kufika hatua ili kila mtu aliyepewa wajibu aogope kuwasababishia hasara watu wengine…

Ishu ya vijana kugombea nafasi za uongozi; “ Mwenyekiti yeye anachokifanya anatengeneza succession plan ya kuwaandaa vijana ndani y Chama.. Kwenye maeneo mengi Serikali za mitaa vijana wameshinda, karibu kila eneo ambako alisimama mzee na kijana mzee alishindwa… Kilichotumika si ujana, kilichotumika ni kutaka pale pabadilishwe…

Ishu ya kutangaza kugombea Urais; “Tutavuka mto tukifika mtoni..

Likaulizwa swali kuhusu ile skafu yake anayopenda kuivaa; “ni kitu kama kigumu sana kuja kupata vazi moja ambalo litavaliwa na Wamasai, Wanyakyusa, Wazanzibar nadhani ni ngumu sana. Nilichokiona kinaweza kikafaa kwa wote ni skafu, hata mtu aliyevaa kanzu anaweza akaweka skafu. Mama na yeye anaweza akaweka skafu…

Swali la kiongozi gani upande wa upinzani anamvutia; “… Zitto Kabwe, lakini kuchukua nchi bado hata yeye anajua …

Unaweza kuisikiliza sauti yote ya Naibu Waziri huyo kutoka kwenye show ya Mkasi hapa.BOFYA HAPA

Chnazo:-Millardayo.
 
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad