AFCON 2015:-Yaliyojiri Picha wakati Timu ya Algeria ikiitandika Africa Kusini bao 3. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 20, 2015

AFCON 2015:-Yaliyojiri Picha wakati Timu ya Algeria ikiitandika Africa Kusini bao 3.

Mara  baada ya Januari 19,2015,Usiku ,Timu ya Taifa ya  Senegal kuifunga Ghana 2-1 katika Mechi ya kwanza ya Kundi C la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, Estadio de Mongomo iliyopo Mjini Mongomo Nchini Equatorial Guinea, ilishuhudia Mechi nyingine ya Kundi hilo ambapo Algeria, Nchi ambayo ndiyo iko juu kabisa kwa Afrika katika Msimamo wa FIFA wa Ubora Duniani, kutoka nyuma na kuitwanga Africa Kusini Bao 3-1.



Thuso Phala aliipa Bao South Africa, maarufu kama Bafana Bafana, Dakika ya 51 na Dakika ya 55 Tokelo Anthony Rantie akaikosesha Bao la Pili baada ya Penati yake kupiga Posti.

Algeria walisawazisha Dakika ya 67 kwa Bao la kujifunga mwenyewe Thulani Hlatshwayo na kupiga la Pili Dakika ya 72 kupitia Faouzi Ghoulam kisha Slimani akaweka Bao la 3 Dakika ya 83 kufuatia makosa ya Kipa Keet.

Leo Jumanne Januari 20,20115 zipo Mechi mbili za Kundi D huko Mjini Malabo kwenye Uwanja wa Nuevo Estadio de Malabo na ya kwanza ni kati ya Côte d'Ivoire na Guinea ikifuatiwa na ile ya Mali na Cameroon.

Jumanne Januari 20,2015

1900 Côte d'Ivoire v Guinea [Nuevo Estadio de Malabo]  
               
2200 Mali v Cameroon [Nuevo Estadio de Malabo] 
    
Jumatano Januari 21,2015

KUNDI A

1900 Equatorial Guinea v Burkina Faso [Estadio de Bata]  
              
2200 Gabon v Congo [Estadio de Bata]     
      
Alhamisi Januari 22,2015

KUNDI B

1900 Zambia v Tunisia [Nuevo Estadio de Ebebiyín]   

2200 Cape Verde Islands v Congo DR [Nuevo Estadio de Ebebiyín] 
          
Ijumaa Januari 23,2015

KUNDI C

1900 Ghana v Algeria [Estadio de Mongomo]  

2200 South Africa v Senegal [Estadio de Mongomo]  
           
Jumamosi Januari 24,2015

KUNDI D

1900 Côte d'Ivoire v Mali [Nuevo Estadio de Malabo] 

2200 Cameroon v Guinea [Nuevo Estadio de Malabo]  
        
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad