Anatakiwa
ajue siku ileile kwamba hakuna dhamana, taratibu za kimahakama zitaendelea
akiwa ndani nakutoka hapo adhabu yake inatakiwa imtishe… Kama mtu amesababisha
hasara ya bilioni thelathini, kama adhabu nii kumuondoa tu kwenye nafasi
aliyokuwa nayo umempa likizo akatumie fedha… Umempa send-off akasherekee fedha
ya umma…”– Mwigulu
Nchemba.
Kuhusu hatua
ambazo zimefikiwa mpaka sasa kwa wale waliochukua pesa za Escrow, Naibu
Waziri huyo alisema; “Taarifa nilizonazo tayari Mamlaka ya Mapato
imeshafanya hesabu… Kuhusu haya mambo ya Kodi kweli tumedhamiria, kwamba lazima
kodi ilipwe na hili si jambo la mjadala… Hatuwezi tukasamehe kodi kubwa vile
halafu tukakimbizana na mama anayeuza mchicha…”– Mwigulu Nchemba.
Alipoulizwa
kuhusu msimamo wake kwenye Uchaguzi 2015 alijibu; “Ninataka nifocus sana
kumsaidia Waziri kwenye haya majukumu ambayo tumepewa na Mheshimiwa Rais
kuhakikisha kwamba Serikali inatimiza wajibu wake… Nikirudi kwenye Chama
namsaidia Katibu Mkuu kusimamia misingi ya Chama…
Nisingependa niwe miongoni
mwa wanaovunja miiko.. Tutavuka mto tukishafika mtoni kufuatana na taratibu
zetu…”– Mwigulu Nchemba.
Msimamo
wangu kwenye masuala ya msingi yanayohusu taifa letu huwa hauyumbi
wanaonifahamu wanajua…”
|
No comments:
Post a Comment