FIFA Ballon d'Or 2014:-Hii ndio Taswira ya Jinsi kura zilivyopigwa Kumchagua Ronaldo kwa Mwaka wa Pili mfululizo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 13, 2015

FIFA Ballon d'Or 2014:-Hii ndio Taswira ya Jinsi kura zilivyopigwa Kumchagua Ronaldo kwa Mwaka wa Pili mfululizo.

Cristiano Ronaldo, kwa Mwaka wa Pili mfululizo ameshinda FIFA Ballon d'Or ambayo ni Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2014 na kuwafunika Wapinzake wake Lionel Messi na Manuel Neuer.

Ronaldo alitangazwa Mshindi kwenye Hafla iliyofanyika Jana Januari 13,2015 huko Ukumbi wa Kongresshaus Jijini Zurich huko Uswisi na hii ni mara ya 3 kwake kuizoa Tuzo hii ambayo Messi anaongoza kwa kuitwaa mara 4.

Mara ya kwanza Ronaldo kutwaa Tuzo hiyo ilikuwa Mwaka 2008 wakati alipokuwa akiichezea Manchester United.
KURA ZA TANZANIA.

KURA
NCHI
JINA
1
2
3
KOCHA
TANZANIA
NOOIJ MART
ROBBEN ARJEN
MESSI LIONEL
CRISTIANO RONALDO
KEPTENI
TANZANIA
HAROUB NADIR
MESSI LIONEL
CRISTIANO RONALDO
MUELLER THOMAS
MWANAHABARI
TANZANIA
WAMBURA BONIFACE
CRISTIANO RONALDO
MESSI LIONEL
MUELLER THOMAS

TAZAMA MGAWANYO WA KURA ZOTE KWA WACHEZAJI WOTE.

Chati inavyoonyesha kura walizopigiwa wachezaji waliokuwa wanawania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia jana mjini Zurich, Uswisi. Cristiano Ronaldo aliwashinda Lionel Messi, Manuel Neuer, Arjen Robben na Thomas Muller na kubeba Ballon d'Or ya FIFA kwa mara ya pili mfululizo.



Kiungo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa na mshindi wa Kombe la Dunia 1998, Christian Karembeu (kushoto) akimkabidhi James Rodriguez tuzo ya Bao Bora la Mwaka, maarufu kama Puskas usiku huu mjini Zurich, Uswisi. Mshambuliaji huyo wa Real Madrid amewapiku Stephanie Roche na Robin van Persie.

Rodriguez akiwasili na mkewe Daniela Ospina

Nae kocha wa Ujerumani, Joachim Low (Pichani ) ametajwa kuwa kocha Bora wa Mwaka wa Dunia katika sherehe za FIFA utoaji tuzo za Mwanasoka Bora wa Dunia zinazoendelea mjini Zurich, Uswisi.

Low amewapiku makocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti na Atletico, Diego Simeone kushinda tuzo hiyo baada ya kuiongoza Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia nchini Brazil kwa mara ya nne mwaka jana 2014.  

Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 54 aliisaidia Ujerumani kumaliza ukame wa miaka 18 wa kusubiri taji hilo kwa kuifungaArgentina katika Fainali, bao pekee la Mario Gotze dakika za nyongeza.PICHA ZAIDI NA NAMNA TUZO HIZO ZILIVYOTOLEWA BOFYA HAPA

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad