EPL 2014/2015:-Matokeo ya leo Januari 31,2015....Liverpool 2-0 West Ham..huku RVP and Falcao wakiipaisha Manchester United Nafasi ya 3. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 31, 2015

EPL 2014/2015:-Matokeo ya leo Januari 31,2015....Liverpool 2-0 West Ham..huku RVP and Falcao wakiipaisha Manchester United Nafasi ya 3.

Manchester United Leo Januari 31,2015 wameitandika Timu ya mkiani Leicester City Bao 3-1 Uwanjani Old Trafford na kukamata Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu Uingereza 2014/2015.

Manchester United walipata Bao la Kwanza kwenye Dakika ya 27 baada ya Daley Blind kumtengenezea Mfungaji Robin van Persie na Bao la Pili kuja Dakika ya 32 kufuatia Shuti la Angel Di Maria kumaliziwa na Radamel Falcao.

Dakika ya 44, Man United walifunga Bao la 3 baada ya Wes Morgan kujifunga mwenyewe.

Katika Dakika ya 80, Marcin Wasilewski alifunga Bao pekee la Leicester kwa Kichwa.

Huko Anfield, Liverpool waliichapa West Ham Bao 2-0 kwa Bao za Raheem Sterling, Dakika ya 51, na Daniel Sturridge, Dakika ya 80.

Sturridge, ambae alikuwa nje ya Uwanja kwa Miezi Mitano baada ya kuumia, aliingizwa Dakika ya 68 kumbadili Markovic na hii ilikuwa ni Mechi yake ya kwanza kabisa.


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad