AFCON 2015:-Matokeo ya Mechi zote Januari 17 na Leo Januari 19,2015 kwa Ghana kubondwa 2-1 na Senegal . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 19, 2015

AFCON 2015:-Matokeo ya Mechi zote Januari 17 na Leo Januari 19,2015 kwa Ghana kubondwa 2-1 na Senegal .

Usiku wa leo Januari 19,2015 huko Estadio de Mongomo, Mjini Mongomo Nchini Equatorial Guinea, Senegal ilitoka nyuma na kuiangusha Ghana Bao 2-1 kwenye Mechi ya Kundi C la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, huku Bao la ushindi likifungwa Dakika za Majeruhi.

Ghana walitangulia kufunga kwa Penati ya Dakika ya 14 Andre Ayew iliyotolewa baada Kipa wa Senegal, Coundoul, kumwangusha Atsu.

Senegal walisawazisha kwa Bao la Dakika ya 58 la Straika wa zamani wa Manchester United ambae sasa anachezea Stoke City, Mame Briam Diouf, na kufunga Bao la Pili na la ushindi baada ya Dakika 90 kumalizika katika Dakika za Majeruhi kupitia Moussa Sow.



Add caption

Mechi nyingine ya Kundi B la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, kati ya Cape Verde na Tunisia ilimalizika 1-1 kama ilivyokuwa kwa nyingine ya Kundi hilo iliyochezwa mapema Jana Januari 18,2015 kwisha 1-1 kati ya Zambia na Congo DR.

Mechi zote hizo zilichezwa Nuevo Estadio de Ebebiyín , Mjini Ebebiyin.
Kwenye Mechi ambayo kila Timu ilikosa Mabao ya wazi, Mohamed Ali Moncer aliipa Tunisia Bao la kuongoza katika Dakika ya 70 na Almeida Heldon kusawazisha kwa Penati Dakika 7 baadae.


Baadae hii Leo, hapo hapo Estadio de Mongomo, Mjini Mongomo, ipo Mechi ya pili ya Kundi C kati ya Algeri a na South Africa.

AFCON 2015  RATIBA/MATOKEO.

Jumamosi Januari 17,2015.

Equatorial Guinea 1 – 1  Congo      
Burkina Faso 0 – 2 Gabon 

Jumapili Januari 18,2015.

Zambia 1 – 1 Congo DR
Tunisia 1 – 1 Cape Verde Islands 
            
Jumatatu Januari 19,2015.

Ghana 1 – 2 Senegal            
2200 Algeria v South Africa [Estadio de Mongomo]  
  
Jumanne Januari 20,2015.

1900 Côte d'Ivoire v         Guinea [Nuevo Estadio de Malabo]                 
2200 Mali v Cameroon [Nuevo Estadio de Malabo]   
  
Jumatano Januari 21,2015.

1900 Equatorial Guinea v Burkina Faso [Estadio de Bata]                
2200 Gabon v Congo [Estadio de Bata]    
       
Alhamisi Januari 22,2015.

1900 Zambia v Tunisia [Nuevo Estadio de Ebebiyín]   
2200 Cape Verde Islands v Congo DR [Nuevo Estadio de Ebebiyín]   
        
ROBO FAINALI

Jumamosi Januari 31,2015.

1900 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Estadio de Bata]==RF1  
2200 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Nuevo Estadio de Ebebiyín]==RF2

Jumapili Februari 1,2015.

1900 Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Estadio de Mongomo]==RF3   
2200 Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Nuevo Estadio de Malabo]==RF4  
     
NUSU FAINALI

Jumatano Februari 4,2015.

2200 RF 1 v RF4 [Estadio de Bata]==NF1   
    
Alhamisi Februari 5,2015.

2200 RF2 v RF3 [Nuevo Estadio de Malabo]==NF2 
   
MSHINDI WA TATU.

Jumamosi Februari 7,2015.

2100 Aliefungwa NF1 v Aliefungwa NF2 [Nuevo Estadio de Malabo]

FAINALI

Jumapili Februari 8,2015.

2200 Mshindi NF1 v Mshindi NF2 [Estadio de Bata]    


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad