ULINZI SHIRIKISHI NYAKAHURA:-Walinzi Watishia Kugoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, December 31, 2014

ULINZI SHIRIKISHI NYAKAHURA:-Walinzi Watishia Kugoma.

Pichani ni Askari wa Kikundi cha ulinzi kinacholinda raia  na mali zao katika vijiji vya Ngalalambe na Muhongola kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo mkoani Kagera wakiwa mbele ya wananchi wa vijiji hivyo kutaka msimamo wa kuendelea na kazi yao  ya kuwasaka wahalifu wakati wa mchana na usiku.:..Picha na Shaaban Ndyamukama.

Kikundi cha ulinzi kinacholinda raia  na mali zao katika vijiji vya Ngalalambe na Muhongola kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo mkoani Kagera kimesitisha kazi yake baada ya vijana wa kikundi hicho kutishiwa maisha wakati wa usiku.

Mwenyekiti wa kikundi hicho,Bw.Kabika Tilukenzile ametoa taarifa hiyo Desemba 30,2014, kwenye mkutano wa  wajasiliamali wa Nyakahura - Muzani na kwamba wanaotishiana maisha ni walinzi wa maduka ya wafanyabiashara, katanani humo.
  
Bw Tilukenzile amesema walinzi wake wamesitisha shughuli ya doria na kudhibiti wahalifu ili kulinda  maisha yao na walinzi wa maduka ndio wadhibiti maeneo yote ya wananchi katika vijiji hivyo kuhakikisha usalama unaendelea kuwepo.

Sisi kazi yetu ni kulinda wananchi na mali zao kwa kushirikiana na jeshi la polisi na wahalifu wanapokamatwa wanafikishwa kwenye sheria lakini kwa kuwa tumeanza kutishiwa ni bora tusalimishe maisha”.-amesema Tilukenzile
Hata hivyo wananchi na wajasiliamali katika vijiji hivyo wamewataka vijana hao kufanya kazi kwa kujiamini kuliko kutishiwa na walinzi wa maduka ya wafanyabiashara wakubwa ambao wako chini ya mtu kwa maslahi yake binafsi.

Mmoja  wa wananchi na mjasiliamali Bw.Pastory Rwabukoba amesema kikosi cha walinzi wa maduka katika vijiji hivyo kinachotishia kikundi cha walinzi shirikishi kinachochewa na viongozi wa kisiasa ambao hawana budi kudhibitiwa.

Amesema ulinzi shirikishi ulianzishwa na wanaharakati wa CHADEMA na kuungwa mkono na wananchi wote na kudhibiti uhalifu tangu Aprili mwaka jana(2013) hali iliyochangia kuleta usalama katika eneo hil.

Mwenyekiti wa kijiji cha Ngalalambe ,Bw.Yusufu Seif na Mwenyekiti wa wajasiliamali Nyakahura - Muzani Bw.Jackson Muganyizi wameahidi kutatua mgogoro huo wakishirikisha kamati ya ulinzi na usalama ngazi ya kata.

Kikundi cha walinzi shirikishi cha Nyakahura - Muzani kinao vijana 20 wanaolipwa kiasi cha Sh.1.2 milioni kwa mwezi na wajasiliamali wa vijiji hivyo na kimepongezwa kwa kudhibiti wahalifu hasa waliojihusisha na udokozi vibandani.
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad