MAAJABU :-Miezi 9 hakuna majibu ya ndege ya Malaysia Airlines 370, nyingine imepotea Desemba 28,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 29, 2014

MAAJABU :-Miezi 9 hakuna majibu ya ndege ya Malaysia Airlines 370, nyingine imepotea Desemba 28,2014.

Bado Dunia imebaki njia panda juu ya wapi ilipo ndege ya Malaysia Airlines 370 ambayo ilikuwa na abiria 239, ilipotea miezi zaidi ya nane iliyopita ikitokea Malaysia kwenda China, ndege nyingine imepotea, ilitokea Singapore kwenda Indonesia.

Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Desemba 28,2014, Jumapili imeendelea leo Desemba 29,2014 tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Watu 162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege.

Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia. Shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.

Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.

Airasia iliotoweka Desemba 28,2014 Pichani ni AirAsia qz 8501, ilikuwa na abiria 162 wengi wao walikuwa raia wa Indonesia na Uingereza na ilipotea wakati rubani alipolazimika kubadili mwelekeo wa ndege hiyo pasipo kuomba mwelekeo kutoka kwa waongozaji kutokana na hali mbaya ya hewa.
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad