Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) itaingia raundi ya tisa Januari 3 mwakani kwa mechi tano,kwa Coastal
Union itacheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mkwakwani, Ruvu Shooting
itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Azam itakuwa mwenyeji wa
Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Azam Complex, Stand United itakuwa mgeni wa
Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati Mbeya City na Yanga
zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Sokoine.
Ligi hiyo
ambayo itachezwa mfululizo (non-stop) hadi itakapomalizika Mei 9 mwakani,
itakamilisha raundi ya tisa Januari 4 mwakani kwa mechi kati ya Mgambo Shooting
na Simba kwenye Uwanja wa Mkwakwani, na Tanzania Prisons itakayokuwa mwenyeji
wa Ndanda kwenye Uwanja wa Sokoine.
Nayo mechi
kati ya Mtibwa Sugar na Stand United ambayo jana ilivunjwa na mvua dakika ya 6
imemaliziwa leo ambapo timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Wakati huo
huo, mechi ya ligi iliyochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex
imemalizika kwa wageni Ruvu Shooting kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT
Ruvu. Bao hilo lilifungwa kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na
Hamisi Kasanga.
UNGANANASI
KATIKA FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment