Aidha pamoja
na kupungua kwa samaki nchini lakini
nguvu ya uvuvi imeongezeka kutoka wavuvi 182,741 waliotumia vyombo vya uvuvi
56,985 mwaka 2012 hadi wavuvi 183,431 waliotumia vyombo vya uvuvi 57,385 mwaka
2013.
Katika
kilele hicho cha maadhimisho ya siku ya uvuvi duniani pia wavuvi walitoa
changamoto wanazokabiriana nazo katika kuteleza majukumu yao kama kuvamiwa na
maharamia ziwani wakivua, halamashauri za Wilaya kutotenga bujeti za
kuwaendeleza wavuvi, Taasisi za kifedha kutotambua uwekezaji wa wavuvi ili
kuwapatia mikopo ya kujiendeleza.
Akijibu
utatuzi wa changamoto hizo Naibu Waziri Telele alisema wizara yake imeandaa na
kuanza kutekeleza program ya kuendeleza sekta ya uvuvi kwa kipindi cha mwaka
2011/2012 hadi mwaka 2015/2016, Programu hiyo inajumuisha mambo makubwa
manne yafuatayo.
Usimamizi
endelevu wa rasilimali za uvuvi, Matumizi endelevu ya rasilimali uvuvi na
masoko, tatu Uendelezaji wa ukuzaji wa viumbe kwenye maji na , nne Utafiti wa
huduma za mafunzo na huduma za ugani ili kuhakikisha sekta ya uvuvi inakua kwa
kasi na kuleta manufaa kwa wananchi walio wengi.
Aidha Naibu
Waziri Telele aliushukuru mfuko wa hifadhi wa NSSF kwa kuingia katika sekta ya
uvuvi na kuanza kuwaelimisha wavuvi na kuwapa maono na elewe kuhusu huduma
zitolewazo na mfuko huo pia alitoa wito kwa mifuko na taasisi nyinginezo
kujikita katika sekta hiyo ili kuinua uchumi wa wavuvi.
|
No comments:
Post a Comment