Jopo la Majaji watatu wa mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam chini ya Jaji Radhia
Sheikhe limezuia mjadala wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali
kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow hadi hapo hoja ya msingi ambayo ipo mahakamani
itakapofanyiwa kazi.
Jopo hilo
lililokuwa likiongozwa na Mh Radhia Sheikhe wameagiza kutofanyika kwa mjadala
wotote kuhusu ripoti ya CAG huko bungeni na kuongeza kuwa majadiliano hayo
yanaweza kufanyika baada ya shauri la msingi kupatiwa ufumbuzi.
Awali
akizungumza na ITV mwanasheria wa IPTLl wakili Joseph Makandege amesema
wamefikisha shauri hilo namba 50 katika mahakama hiyo wakitaka vifanyike vitu
viwili kwanza kupata tafsiri sahihi ya kisheria kuwa kama kitendo
kilichofanywa na ofisi ya CAG kufanya ukaguzi katika akaunt za Escrow kama ni
sahihi akaongeza kuwa wao wanachoamini ni kuwa kwa sababu jambo hilo lilikuwa
limekwisha amuliwa kisheria mahakama na kwa kutolewa kwa hukumu kulikuwa hakuna
haja tena na bunge kuagiza uchunguzi ufantike.
Aidha mwanasheria
huyo akaongeza kuwa siyo kwamba hawataki jambo hilo kujadiliwa bali wanataka
taratibu zifuatwe ili kuweza kufiki mwafaka wa kina katika jambo hilo
mwanaasheria huyo akaongeza kuwa mbali na kupata tafsiri hiyo ya kisheria pia
wanaiomba mahakama kulitaka bunge kusitisha mpango wake wakujadili tarifa ya
CAG hadi tafsiri ya kina ipatikane.
Mwanasheria
huyo pia akasema kuwa wao wanaona kama likijadiliwa haki haitaweza kutendeka
kwa sababu wao kama IPTL hawana mwakilishi bungeni na hivyo maamuzi yatafanyika
upande mmoja.
Kwa upande
wa jopo la wanasheria wa serikali wakiongozwana Obadia Kaimela wameiomba
Mahakama kuwapa muda wa kuweza kuwasiliana na baadhi ya watu ama taasisi
zinazohusishwa na jambo hilo ili kuweza kupata muda wa kutosha kutoa utetezi
wao.
Kutakana na
hali hiyo imeamuliwa kuwa bada ya kukamilika kwa taribu zote kesi ya msingi
ikiwemo uwasilishwaji wa viapo kesi ya msingi itanza kusikilizwa Desemba 2
mwaka huu.
|
No comments:
Post a Comment