Kikao cha Bunge leo Novemba 27 kimeanza kwa
maswali mawili kuulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman
Mbowe kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
“…Chini ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na ukiwa kiongozi wa shughuli za Kiserikali Bungen,
tumeiona Serikali ikikumbana na matatizo na vikwazo vingi ikiwemo ‘Operesheni
Tokomeza’ ambayo ilipelekea wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata
vilema…“– Mbowe.
Tumeona
mauaji ya raia yakiendelea Kiteto, kashfa kubwa ambayo iko current sasa hivi
ikiwa ni pamoja na kauli zako ulizowahi kuzisema kwamba fedha zilizopotea za
akaunti ya Escrow hazikuwa fedha za umma bali zilikuwa fedha za watu binafsi…“– Mbowe.
Baada ya
Ripoti ya CAG kutolewa hadharani kuhusiana na fedha za Escrow na baada ya
Ripoti ya PCCB kutolewa na hatimaye jana hapa Bungeni kusomwa taarifa ya Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali, nini msimamo wako kuhusu kauli yako ya awali
kwamba fedha zile zilikuwa ni za watu binafsi na sio fedha za umma?“– Mbowe.
Kwa
uzito huo ukichanganya na matukio mengine mbalimbali ambayo yamepelekea fedheha
kubwa kwa taifa letu, huoni kama ingekuwa muafaka kwako binafsi na taifa
kupumzika kidogo ili kupisha nafasi kwa watu wengine kuweza kumalizia ngwe hii
ya utawala wenu?”– Mbowe.
Akijibu maswali
hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema; “…Inawezekana Mheshimiwa Mbowe una shauku ya kutaka litokee
hilo lakini mambo haya yanategemea kama ndivyo Mungu kapanga au hapana…“
Ningeweza
nikajaribu kukujibu lakini sina sababu ya kufanya hivyo, sina sababu ya kufanya
hivyo kwa sababu suala lenyewe ndiyo subject ya mjadala hapa Bungeni ambao
unaanza leo.. Tusubiri mjadala utakavyokwenda naamini na mimi nitapata nafasi
ya kusema mawili matatu, kwa hiyo nadhani mwisho wa yote Bunge litakuwa
limefikia mahali ambapo tunaweza tukasema kwa uhakika ni hatua stahiki namna
gani inaweza kuchukuliwa…” Waziri Mkuu Mizengo
Pinda.
Baada ya majibu
hayo, Mbowe alipata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwa
Waziri Mkuu; “…Pamoja na kwamba jambo hili litajitokeza
baadaye katika mijadala ya leo, bado haiondoi ukweli kwamba una wajibu wa
kulijibu swali langu. Naomba kwa heshima sana nikuulize tena kwa mara nyingine,
taifa limepata fedheha kubwa sana kutokana na sakata hili, nchi nzima
inasikiliza tatizo hili…“– Mbowe.
“…Una heshima kama kiongozi wa Serikali lakini heshima ambayo
itakuwa imethibitishwa zaidi kama utaamua kujiwajibisha mwenyewe ili kuweka
heshima yako na heshima ya Serikali, je kwa mara nyingine huoni ingekuwa vema
kama basi utujibu kama unafikiri bado zile fedha ni za umma kama hutaki ku-declare
kujiuzulu katika hatua ya sasa?”– Mbowe.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu
amesema; “…Naomba nirudie
nilichosema, suala la kujiuzulu si jipya lakini maadam jambo hili liko hapa
Bungeni, unatanguliza hili jambo kwanini? Tungoje tujadili tufikie mwisho halafu
tutaamua…”– Mizengo Pinda.
|
No comments:
Post a Comment