AJALI:-Watu 11 wamefariki dunia wengine 25 kujeruhiwa baada ya basi dogo kugongana uso kwa na lori,wilayani Muheza. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, November 27, 2014

AJALI:-Watu 11 wamefariki dunia wengine 25 kujeruhiwa baada ya basi dogo kugongana uso kwa na lori,wilayani Muheza.

Watu 11 wamekufa na wengine 25 kujeruhi vibaya baada ya basi dogo aina ya Coaster la kampuni ya ''Thende Sheki'' kugongana uso kwa uso na lori la mizigo leo November 27,2014  katika eneo la mkanyageni lililopo wilayani Muheza mkoani Tanga.

Ajali hiyo ilikusanya mamia ya wananchi kutoka jijini Tanga,Muheza na Lushoto kwa ajili ya kwenda kushuhudia na kutambua miili ya marehemu iliyokuwa imehifadhiwa nje katika hospitali teule ya Mtakatifu Augustino wilayani Muheza kwa ajili ya utambuzi ambapo hadi majira ya mchana miili ya watu 9 waliokufa papo hapo katika eneo la tukio ilitambuliwa na ndugu na jamaa.


Akielezea miili na majeruhi waliopokelewa katika hospitali hiyo,kaimu mganga mkuu wa wilaya ya muheza Dkt.Perter Shemkhai amesema watu wawili walifariki hospitali muda mchache baada ya kuletwa na kupatiwa tiba katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamesema dereva mwenye lori alikuwa akiyumba njia nzima kabla ya kukutana uso kwa uso na gari dogo la abiria aina ya Coaster hatua waliyodai kuwa ina viashiria vya dereva wa lori hilo alikuwa amepitiwa na usingizi wakati akiwa barabarani. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad