UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2014/2015:-Picha wakati Magoli 40 yakifungwa October 21, 2014 kwa Chelsea 6, Bayern Munich 7, Shakhtar 7 na FC Barcelona 3. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, October 22, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2014/2015:-Picha wakati Magoli 40 yakifungwa October 21, 2014 kwa Chelsea 6, Bayern Munich 7, Shakhtar 7 na FC Barcelona 3.

Wakicheza kwao Olimpico Stadium Jijini Rome Jana October 21, 2014,kwenye Mechi ya Kundi E, AS Roma wameshushiwa kipigo kitakatifu na Bayern Munich kwa kutandikwa Bao 7-1.

 Bayern walifunga Bao zao katika Dakika ya 8 baada ya Nahodha Phlipp Lahm kumpa pasi Arjen Robben aliachia shuti hadi wavuni.

Bao nyingine za Bayern zilifungwa katika Dakika ya 23 na Mario Gotze, Dakika ya 25 na Robert Lewandowski na Arjen Robben kufanya Bayern 4 AS Roma 0 katika Dakika ya 30.

Bayern walifunga Bao lao la 5 kwenye Dakika ya 35 kwa Penati ya Thomas Muller ambayo ilitolewa kufuatia Manolas kuunawa Mpira.

Gervinho aliipa Bao AS Roma kwenye Dakika ya 66 kufuatia ushirikiano mzuri wa Florenzi na kisha Nainggolan kutumbukiza Krosi iliyounganishwa wavuni kwa Kichwa na Gervinho.

Franck Ribery, alieingizwa badala ya Lewandowski katika Dakika ya 68, aliipa Bayern Bao la 6 Dakika ya 78 na Bao la 7 kwa Bayern kufungwa na Xherdan Shaqiri, aliembadili Mario Gotze katika Dakika ya 79, na Bao hilo liliingia Dakika ya 80.

MSIMAMO.

KUNDI E
KLABU
P
W
D
L
F
A
+/-
Pts
FC Bayern München
3
3
0
0
9
1
8
9
AS Roma
3
1
1
1
7
9
-2
4
Manchester City FC
3
0
2
1
3
4
-1
2
PFC CSKA                            
3
0
1
2
3
-8
-5
 1



Uwanjani Stamford Bridge, Wenyeji Chelsea wameichakaza NK Marbor kwa kuichapa Bao 6-0 katika Mechi ya G.

Chelsea walifungua kitabu cha Magoli Dakika ya 13 baada ya  pasi safi ya John Terry kumfungulia njia Loic Remy aliefunga vizuri na kuipa Chelsea Bao la kuongoza.

Juhudi hiyo ya Remy ilimfanya aumie Nyonga na Dakika chache baadae kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Didier Drogba.

Drogba aliipa Chelsea Bao la Pili katika Dakika ya 22 kwa Penati iliyotolewa baada ya Pasi ya Willian kumgonga mkononi Ales Mertelj.

John Terry aliipa Chelsea Bao la 3 katika Dakika ya 30 kufuatia kaunta ataki safi iliyoanzia kwa Drogba kuokoa Mpira langoni wakati wa Kona na Eden Hazard kukokota Mpira hadi eneo la Maribor na kumpasia Cesc Fabregas aliempa Terry, aliepanda toka Difensi, na kufunga.

Dakika ya 54, Chelsea walipata Bao la 4 la kujifunga wenyewe kufuatia krosi ya Eden Hazard kumgonga kwenye kisigino Mitja Viler na kutinga.

NK Maribor walipata Penati katika Dakika ya 64 iliyotolewa baada ya Nemanja Matic kumchezea Rafu Agim Ibraimi ambae alipiga mwenyewe na kugonga Posti.

Chelsea walifunga Bao la 5 kwa Penati waliyopata baada ya Marko Suler kumshika Branislav Ivanovic na kumwangusha na Penati hiyo kufungwa kifundi na Eden Hazard katika Dakika ya 77.

Dakika ya 90, Eden Hazard aliipa Chelsea Bao la 6 baada kupokea na kutuliza pasi ya juu toka kwa Nathan Ake na kumpunguza Beki mmoja na kufunga.

MSIMAMO.
 
KUNDI G
KLABU
P
W
D
L
F
A
+/-
Pts
Chelsea FC
3
2
1
0
8
1
7
7
FC Schalke 04                 
3
1
2
0
6
5
1
6
NK Maribor
3
0
2
1
2
8
-6
Sporting Clube de Portugal
3
0
1
2
4
6
-2
1
RATIBA/MATOKEO UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2014/2015.

Jumanne Oktoba 21,2014.
  KUNDI E
 
CSKA Moscow 2- 2 Man City 

AS Roma 1 – 7 Bayern Munich

KUNDI F

APOEL Nicosia 0 – 1 Paris St-Germain 

Barcelona 3 – 1 Ajax

KUNDI G

Chelsea 6 – 0 NK Maribor 

FC Schalke 4 – 3 Sporting Lisbon

KUNDI H
 
BATE Borisovs 0 – 7 Shakhtar Donetsk 

FC Porto 2 – 1 Athletic Bilbao

MSIMAMO.

KUNDI F
KLABU
P
W
D
L
F
A
+/-
Pts
Paris Saint-Germain
3
2
1
0
5
3
2
7
FC Barcelona
3
2
0
1
6
4
2
6
AFC Ajax
3
0
2
1
3
5
-2
2
APOEL FC                          
3
0
1
2
1
3
-2
 1

RATIBA/MATOKEO UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2014/2015.

Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku kwa Saa za Bongo.

Jumatano Oktoba 22,2014.

KUNDI A

Atlético Madrid v Malmö FF

Olympiakos v Juventus

KUNDI B

Liverpool v Real Madrid

Ludogorets Razgrad v FC Basel

KUNDI C

Bayer 04 Levserkusen v Zenit St Petersburg

Monaco v Benfica

KUNDI D

Galatasaray v Borussia Dortmund

RSC Anderlecht v Arsenal
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad