SHERIA ZETU:-Tazama Picha 6 za Mazingira ya Gereza atakaloishi Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, October 21, 2014

SHERIA ZETU:-Tazama Picha 6 za Mazingira ya Gereza atakaloishi Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius

Mwanariadha mlemavu, Oscar Pistorius aliyehukumiwa miaka mitano jela,leo October 21,2014, tayari ameingia kwenye gereza kongwe la Kgosi Mampuru II Prison.

Gereza hilo liko jijini Pretoria na linajulikana kutokana na kuwa na sifa ya kuhifadhi vijana watukutu.

Mwanariadha huyo amehukumiwa kutokana na kumuua mpenzi wake bila kukusudia.

TAZAMA  MAZINGIRA YALIVYO...




Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 leo October 21,2014, baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake Reeva Steenkamp enzi za uhai wake.

Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp mwaka uliopita bila ya kukusudia.

Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.

Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa.

Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.

Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.

Upande wa mashitaka unasisitiza afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifgungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.

Picha Na:-SaleheJembe Blog.
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad