UEFA 2014/2015:-Kesho October 21-Chelsea na FC Barcelona kusaka ushindi huku Jumatano ANFIELD Ni LIVERPOOL v REAL MADRID! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, October 20, 2014

UEFA 2014/2015:-Kesho October 21-Chelsea na FC Barcelona kusaka ushindi huku Jumatano ANFIELD Ni LIVERPOOL v REAL MADRID!

UEFA Champions League 2014/2015 inarudi dimbani kesho  Jumanne October 21 na Jumatano October 22, kwa Mechi za 3 za Makundi huku Mabingwa wa Ulaya Real Madrid Jumatano wakitua Anfield kupambana na Liverpool katika Mechi ya Kundi B.

Kwenye Kundi hilo, Real Madrid wapo kileleni baada ya kushinda Mechi zao zote Mbili na wanafuata FC Basel wenye Pointi 3 pamoja na Liverpool na mkiani ni Ludogorets Razgrad ambao hawana Pointi.
Jumanne October 21,2014, Mabingwa wa Uingereza, Manchester City watafungua dimba kwa Mechi ya kwanza kabisa itakayochezwa mapema huko Moscow, Urusi watakapoivaa CSKA Moscow kwenye Mechi ya Kundi E.

Baadae Usiku huo, Chelsea watakuwa kwao Stamford Bridge kucheza na NK Maribor huku Arsenal wao watacheza Jumatano Ugenini huko Uholanzi kwa kuivaa RSC Anderlecht.

UEFA CHAMPIONZ LIGI 2014/2015 RATIBA

Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa
 
Jumanne Oktoba 21,2014.

KUNDI E

1900 CSKA Moscow v Man City

AS Roma v Bayern Munich

KUNDI F

APOEL Nicosia v Paris St-Germain

Barcelona v Ajax

KUNDI G

Chelsea v NK Maribor

FC Schalke 04 v Sporting Lisbon

KUNDI H

BATE Borisovs v Shakhtar Donetsk

FC Porto v Athletic Bilbao

Jumatano Oktoba 22,2014.

KUNDI A
 
Atlético Madrid v Malmö FF

Olympiakos v Juventus

KUNDI B
 
Liverpool v Real Madrid

Ludogorets Razgrad v FC Basel

KUNDI C
 
Bayer 04 Levserkusen v Zenit St Petersburg

Monaco v Benfica

KUNDI D
 
Galatasaray v Borussia Dortmund

RSC Anderlecht v Arsenal

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad