SOKA WILAYA YA NGARA:-Tazama Picha 5 jinsi Dabi ya Ngara mjini ikiwapaisha Ngara Boys FC fainali October 26, 2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, October 22, 2014

SOKA WILAYA YA NGARA:-Tazama Picha 5 jinsi Dabi ya Ngara mjini ikiwapaisha Ngara Boys FC fainali October 26, 2014.

Ligi Daraja la nne wilaya ya Ngara mkoani Kagera imeendelea tena leo October 22,2014 ikiwa  ni Hatua ya Nusu fainali ya kwanza katika dimba la Kokoto na ambayo ilikua Dabi ya Mjini Ngara kwa kuwakutanisha Ngara Stars dhidi ya Ngara Boys FC.


Kila upande ulijigamba kumfunga mwenzake katika mchezo huo ,Lakini walikua ni Ngara Boys FC kupitia kwa mchezaji wao Father Joseph aka Prezdaa kuifungia bao 1-0 na kuipaisha sasa hadi Fainali ya Ligi hiyo itakayotoa Bingwa wa wilaya hapo October 26,2014 ambaye pamoja na zawadi ataiwakilisha wilaya ya Ngara katika Ligi Ngazi ya mkoa wa Kagera.

Kesho October 23,2014,Walimu FC watashuka katika uwanja huo kuwakabili Benaco Stars waliokutana nao katika robo fainali na kutoshana ubavu wa bao 3-3 kisha Kuwatoa kwa Penati 5-3.


Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad