REDD'S MISS TANZANIA 2014:-Fahamu Jambo hili Muhimu kumhusu Sitti Mtemvu aliyekuwa Miss Temeke 2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, October 14, 2014

REDD'S MISS TANZANIA 2014:-Fahamu Jambo hili Muhimu kumhusu Sitti Mtemvu aliyekuwa Miss Temeke 2014.

Je, ulikua unafahamu kuwa Mshindi wa Taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu ni mtoto wa damu kabisa wa Mbunge wa wilaya ya Temeke Mh.Abass Mtemvu? kama ulikua haufahamu basi fahamu kuanzia sasa.

 Sitti Mtemvu alivishwa Taji hilo siku ya Jumamosi October 11,2014 na kuvuta kitita cha Shilingi Millioni 18.

Katika shindano hilo lililofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, nafasi ya pili ilikwenda kwa Lilian Kamazima ambaye alijishindia shilingi milioni 6 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Jihan Dimachk aliondoka na fedha tasilimu shilingi Milioni 4.2.

Dorice Mollel alishika nafasi ya nne wakati Nasreen Abdul akichukua nafasi ya tano.
Siti Mtemvu (Redd's Miss Tanzania 2014 ) akiwa na anyedaiwa ni Baba yake, Mbunge wa Temeke (CCM), Abbas Mtemvu.
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad