KUZAMA KWA MITUMBWI KIGOMA:- Jana October 13,2014, asubuhi miili ya watu 7 yapatikana na kwamba Juhudi zinaendelea kuwatafuta wengine. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, October 14, 2014

KUZAMA KWA MITUMBWI KIGOMA:- Jana October 13,2014, asubuhi miili ya watu 7 yapatikana na kwamba Juhudi zinaendelea kuwatafuta wengine.

Wanajeshi wa Jeshi la Wananch (JWTZ) wakiendelea na zoezi la kuopoa miili ya watu waliopata ajali ya mitumbwi katika kijiji cha Kalalangabo baada ya Mitumbwi waliyokuwa wakisafiria kuzama Jumamosi October 11, 2014.

 Zoezi la kutafuta miili ya watu waliofariki kutokana na ajali ya kuzama kwa Mitumbwi katika Ziwa Tanganyika eneo la kijiji cha Kalalangabo linaendelea.

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limesema waokoaji wanaoendelea na zoezi hilo, jana October 13,2014, asubuhi wamepata miili ya watu 7 na kwamba juhudi zinaendelea kuwatafuta wengine.
Pichani juu na chini ni Waokoaji wakiwa wamebeba mwili uliopatikana kutoka ziwa Tanganyika baada ya ajali ya Mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Bw Dismas Kisusi amewataja waliopatikana leo asubuhi wakiwa tayari wamefariki kuwa ni Masoud Ally, Rehema Kassim, Fitina Issa, Hawa Lwampata, Jackob Rashidi, Mohamud Ulimwengu na Hawa Gamba

Kamanda Kisusi amesema zoezi la uokoaji linafanywa kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi JWTZ pamoja na wavuvi na kwamba haijafahamika idadi ya watu ambao bado hawajapatikana

Mitumbwi hiyo imepata ajali juzi Jumamosi na kwamba kwa kawaida hupakia watu 20 lakini inadaiwa kuwa ilikuwa na watu zaidi ya 70 hali iliyosababisha kuzama baada ya kukutana na dhoruba muda mfupi baada ya kuanza safari kuelekea kijiji cha Kigalye mwambao wa ziwa Tanganyika


Viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika eneo la ajali wakiangalia zoezi la upoaji wa miili iliyopatikana katika ziwa Tanganyika kufuatia ajali ya Mitumbwi iliyotokea Jumamosi October 11,2014. 

Nao ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Mstaafu Issa Machibya (wa pili kushoto) anayefuata ni Katibu Tawala wa Mkoa John Nduguru na Ramadhani Maneno Mkuu wa Wilaya ya Kigoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Kigoma.

Aidha  Mkoa wa Kigoma, Luteni Mstaafu Issa Machibya amesema idadi kubwa ya miili  bado iko majini na kuwa zoezi la uokoaji,  linakuwa gumu sababu ya uhaba wa waokoaji pamoja na miundombinu duni ambavyo ni kikwazo na kusisitiza kuwa kazi ya uokoaji inaendelea. 

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad